*************
NJOMBE
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani Njombe TAKUKURtU imemfikisha mahakamani mkazi mmoja wa kijiji cha Ninga anaefahamika kwa jina Josephat Ngimbuzi kwa kosa la kutoa taarifa za uongo TAKUKURU na kwa watumishi wengine wa umma hatua ambayo imeleta taharuki na usumbufu kwa wahanga taarifa hiyo ya uongo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Njombe Domina Mukama amesema siku chache zilizopita mtuhumiwa aliripoti katika taasisi hiyo akidai kwamba afisa mtendaji wa kijiji cha Ninga pamoja na kaimu afisa mtendaji wa kata ya Ninga iliyopo wilayani Njombe wamemuomba rushwa ya shilingi laki 216,000 ili wasimpeleke polisi kwa kosa la kutojenga choo bora nyumbani kwake .
Kufuatia taarifa hiyo takukuru ilitengeneza mtego na kuwatia nguvuni watendaji hao mara tuu baada ya makabidhiano nakuanza uchunguzi watukio hilo ambapo baadae walibaini kuwa taarifa hiyo haina ukweli na badala yake fedha iliyochukuliwa ni ya faini,michango ya shule ya msingi , sekondari na choo ambayo imekuwa ikikwepwa na mtuhumiwa huyo tangu 2017.
Mtandao huu umemtafuta afisa mtendaji wa kijiji Fatma Mnyangwa na pamoja mratibu msaidizi wa kampeni ya Nyumba ni choo katika halmashauri ya wilaya ya Njombe Evelin Kidenya ambao wanathibitisha kutokea mkasa huo na kukana tuhuma za kuchukua rushwa kama inavyoelezwa na mtuhumiwa na kutoa ufafanuzi kwamba fedha iliyochukuliwa ilikuwa ni chango wa ujenzi wa shule ya msingi na sekondari,faini ya kuchelewa kujenga choo kulipa michango ya maendeleo pamoja na kutishia watumishi wa umma.
Wakati takukuru ikichukua hatua hizo kwa mtuhumiwa nao baadhi ya wananchi akiwemo Kasanga Makweta wanaonyesha kufurahishwa na hatua ya kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo kwa madai yankwamba anakwamisha jitihada za serikali za usafi wa mazingira