Msemaji wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Erasto Ching’oro (kushoto) pamoja na wakizungumza na vyombo vya habari kuhusu zoezi la uhuishaji Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Mkoani Kilimanjaro kulia ni Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Kilimanjaro Bi Hilda Lauo
Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
***************
Na Mwandishi Wetu. Kilimanjaro
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa Kanda ya Kasikazini yamehimizwa kujitokeza kwa wingi ikiwa ni mwendelezo wa uhuishaji wa Mashirika yaliyosajili awali kwenye chini ya Sheria nyingine lakini zinafanya kazi za kijamii hivyo kutakiwa kusajili kwa Sheria ya NGOs kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na.3 ya Mwaka 2019.
Akizungumza na vyombo vya habari leo Mkoani Kilimanjaro Msemaji wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Erasto Ching’oro amesema zoezi hilo litafanyika katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro kuanzia tarehe 29, July hadi tarehe 6 Augosti 2019 ili kutoa fursa kwa wadau wa Mashirika yaliyoko Mikoa ya Kasikazini kufanya usajili kwa haraka lakini ikiwa ni nia njema ya Serikali kupeleka huduma karibu na Wananchi.
Bw. Ching’oro ameongeza kuwa NGOs zote zinazofanya kazi za kijamii ambazo awali usajili wake ulifanyika katika Mamlaka nyingine kama RITA, Msajili wa Jumuiya za Kijamii wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na BRELA usajili wake utakuwa umefutwa kama zitashindwa kujisajili chini ya Sheria ya NGOs kama iliyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3 ya mwaka 2019 katika kipindi cha miezi miezi miwili toka tarehe 01 Julai, 2019.
“Sheria inayataka Mashirika hayo kujisajili katika Sheria ya NGOs kwa kipindi cha miezi miwili hivyo huu ni wakati wa Mashirika kujitahimini yako wapi ili yaweze kufanya uamuzi sahihi kabla ya kipindi kilichotolewa na Sheria hii kupita.’’ Alisisitiza Bw. Ching’oro
Bw.Ching’oro amesema usajili huu unafanyika kwa mikoa ya Kanda ya Kaskazini yenye mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara na kutoa wito kwa Mashirika yaliyopo katika Mikoa hiyo kufanya usajili huo akiongeza kuwa zoezi hili linafanyika bila malipo kwa Mashirika yanayouhisha usajili lakini Mashirika yanayojisajili mara ya kwanza yanatoa malipo kwa ajili ya huduma hiyo.
Aidha Msajili Msaidizi Mkoa wa Kilimanjaro Bi Hilda Lauo ameyataka Mashirika Mkoani Kilimanjaro kuhakikisha yanashiriki usajili huu kwani baadhi ya Mashirika Mkoani humo yamekuwa yakitoa huduma za kijamii wakati yakiwa yamesajili katika Sheria nyingine.
“Kuna Mashirika hapa Mkoani yanatoa huduma za Mikopo kwa jamii lakini ukiongea nao wanakwambia tumesajili Brela wakati huduma wanazotoa ni za kijamii hivyo nivyema wafike kwa ajili ya kufanya usajili kwa mujibu wa sheria mpya” alisema Bi. Hilda.
Zoezi hili la usajili limeanza tangu tarehe 10 mwezi huu Jijini Dar es Salaam ambapo asilimia 80 ya NGOs zilizoko Kanda ya Mashiriki zimefanya usajili wake na zoezi la usajili linaendelea kwa kipindi cha miezi miwili kama ilivyo matakwa ya sheria.