Home Siasa ZITTO AMEMTAKA WAZIRI JAFFO KUSIMAMIA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA HAKI

ZITTO AMEMTAKA WAZIRI JAFFO KUSIMAMIA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA HAKI

0

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Bw.Zitto Kabwe akiwaongozi wanachama wa chama hicho pamoja na viongozi katika ufunguzi wa matawi 10 ya Chama hicho katika Kata ya Vingunguti Jijini Dar es Salaam.

Bw.Maalimu Seif akikata utepe kuashiria kufungua matawi ya Chama hicho katika kata ya Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo.

Bw.Maalimu Seif akiongea na wanachama baada ya kufungua moja ya tawi la Chama cha ACT-Wazalendo katika ufunguzi wa Matawi ya chama hicho Jijini Dar es Salaam

*******************

NA EMMANUEL MBATILO

Kiongozi wa Chama Cha ACT- wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini Mh.Zitto Kabwe, amemtaka Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),Mh.Selemani Jafo kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa mujibu na taratibu zilizowekwa pasipo kukiuka utaratibu ili wananchi waweze kumchagua kiongozi wao ambaye watamchagua.

Ameyasema hayo leo akiwa anafungua matawi 10 ya chama hicho akisindikizwa na muenezi wa chama hicho Bw. Seif Sharif Hamad pamoja na viongozi wengine wa chama hicho katika kata ya Vingunguti jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wananchi wa kata ya Vingunguti Jijini Dar es Salaam, amesema kuwa mkakati ambao wameupanga ni kuhakikisha masuala ya haki na uchumi unakuwa katika hali ya kuridhisha hapa nchini.

Aidha Zitto amesema kuwa lengo ni kuhakikisha kata ya Vingunguti kuongozwa na viongozi wa ACT-Wazalendo hivyo ameviomba vyama na visitumie mabavu katika Uchaguzi ujao ili kuweza kutenda haki kwa wapiga kura na wananchi kwa ujumla paspo buguza.