Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Shaibu Nnunduma kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Mwenge huo wa Uhuru leo umekimbizwa katika wilaya ya Kisarawe na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali

(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWEBLOG-KISARAWE)

Kiongozi  wa Mbio za Mwenge Kitaifa ,Mzee Mkongea Ali akimzsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh. Jokate Mwegelo wakati akitoa hotuba fupi ya kupokea mwenge wa Uhuru kwenye uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam  leo  ukitokea Mafia Kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Kisarawe  Bw Mtela Mwampamba.

Kiongozi  wa Mbio za Mwenge Kitaifa ,Mzee Mkongea Ali  akimsikiliza Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. Suleiman Jafo mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika kituo cha afya cha Homboza wilayani Kisarawe ambapo mwenge wa Uhuru umekagua kituo hicho na kuridhika na ujenzi wake,

Kiongozi  wa Mbio za Mwenge Kitaifa ,Mzee Mkongea Ali akimpongeza Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. Suleiman Jafo mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika kituo cha afya cha Homboza wilayani Kisarawe ambacho kimekamilika katikati ni Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh. Jokate Mwegelo.

Kiongozi  wa Mbio za Mwenge Kitaifa ,Mzee Mkongea Ali akiweka jiwe la msingi katika kituo cha afya cha Homboza wilayani Kisarawe ambacho kimekamilika huku Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. Suleiman Jafo akishuhudia

Kiongozi  wa Mbio za Mwenge Kitaifa ,Mzee Mkongea Ali na na wakimbiza mwenge wenzake wakikagua daraja la daraja la Kwa Konzo kata ya  Msimbu wilayani Kisarawe

Kiongozi  wa Mbio za Mwenge Kitaifa ,Mzee Mkongea Ali na Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Suleiman Jafo wakifunua kitambaa kama ishara ya kuweka jiwe la msingi katika  daraja la Kwa Konzo  Kata ya Msimbu wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo na kulia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani Mh.Zainab Vullu.

Kiongozi  wa Mbio za Mwenge Kitaifa ,Mzee Mkongea Ali akimpongeza Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. Suleiman Jafo mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa daraja la Kwa Konzo kata ya Kata ya Msimbu wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo na kulia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani Mh.Zainab Vullu.

……………………………………………………….

NA MWAMVUA MWINYI,MAFIA
KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa ,Mzee Mkongea Ali amesita kufungua na kuweka jiwe la msingi miradi mitatu wilayani Mafia ,mkoani Pwani na kutoa wiki mbili kwa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) kuchunguza miradi hiyo ,thamani yake halisi na matumizi kisha apelekewe taarifa .
Miradi hiyo ni pamoja na hospital ya wilaya ambayo ilitolewa kiasi cha sh.mil 403.600 .
Mradi mwingine ni ujenzi wa barabara ya KN52 Kilimahewa yenye thamani ya mil.22.336 ambayo kalavati na barabara haina ubora pamoja na uendelevu wa mradi wa maji huko Bweni ambako kero za wananchi hazijafanyiwa kazi kipindi kirefu .
Akielezea juu ya hali hiyo iliyojitokeza ,Mkongea alisema endapo kutabainika kuna ubabaishaji juu ya miradi hiyo basi hatua za kisheria zitachukuliwa.
“Tunapitia miradi hii,tunakagua sio tuu kupitia ila ni kujiridhisha ,hivyo basi TAKUKURU na mkuu wa wilaya fuatilieni suala hili kwa kina ,ili kama kutabainika hakuna ubadhilifu mkuu wa wilaya ataifungua miradi hiyo hapo baadae”alifafanua Mkongea.
Nae mkuu wa wilaya ya Mafia ,Shaibu Nnduma alipokea maelekezo na maagizo waliyopatiwa .
Alisema ,jumla ya miradi nane yenye thamani zaidi ya bilioni sita imepitiwa na mwenge wa Uhuru lakini miradi mitatu ndio imewaletea mushkeri.
Mwenge huo baada ya kumaliza mbio zake wilayani Mafia Julai 27 ,umekabidhiwa wilayani Kisarawe na kupokelewa na mkuu wa wilaya hiyo, Jokate Mwegelo Julai 28 na kukimbizwa umbali wa km153.1 .
Akielezea kuhusu miradi iliyopitiwa na mwenge wa Uhuru ,Jokate alieleza miradi mitatu imewekwa jiwe la msingi,minne imekaguliwa na miwili imezinduliwa huku ikiwa imegharimu kiasi cha sh. bilioni 11.97 .