Mkurugenzi wa Katiba na Ufuatiliaji Haki Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Patience Ntwina (kushoto) akizungumza kitu na Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bw. Jumanne Sagini (katikati) huku Dkt. James Jessy (kulia) muendeshaji wa majadiliano akiwasikiliza.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bw. Jumanne Sagini akizungumza na Washiriki wa majadiliano ya pamoja ya kufanyia maboresho mfumo wa haki jinai nchini (hawako pichani)majadiliano hayo yanaendelea jijini Dodoma.
Washiriki wa majadiliano ya pamoja ya kufanyia maboresho mfumo wa haki jinai nchini yanayoendelea jijini Dodoma wakimsikiliza Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bw. Jumanne Sagini (hayupo pichani) aliyekuwa akizungumza na wataalamu hao juu ya kazi ya maboresho ya mfumo wa haki jinai nchini.
Washiriki wa majadiliano ya pamoja ya kufanyia maboresho mfumo wa haki jinai nchini yanayoendelea jijini Dodoma wakimsikiliza Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bw. Jumanne Sagini (hayupo pichani) aliyekuwa akizungumza na wataalamu hao juu ya kazi ya maboresho ya mfumo wa haki jinai nchini.
Mkurugenzi wa Katiba na Ufuatiliaji Haki Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Patience Ntwina (kushoto) akizungumza kitu na Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bw. Jumanne Sagini (katikati) huku Dkt. James Jessy (kulia) muendeshaji wa majadiliano akiwasikiliza.
………………….
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bw. Jumanne Sagini amewataka wataalamu wanaoshiriki majadiliano ya pamoja ya kufanyia maboresho mfumo wa haki jinai nchini kuangalia namna ya kuboresha maeneo ambayo yanawapa mamlaka watu walio katika nafasi za kuzuia uhalifu, ukamataji, uendeshaji wa mashtaka, utoaji adhabu na urekebishaji wa wahalifu kuacha vitendo vinavyowagonganisha wananchi na Serikali.
Bw. Sagini ameyasema hayo jlipokuwa akizungumza na wataalamu wanaoshiriki majadiliano ya pamoja ya kuufanyia maboresho mfumo wa haki jinai yanayoendelea jijini Dodoma kwa ajili ya kuupitia mfumo huo na kuangalia changamoto inazoukabili mfumo huo ili kuona kwa pamoja namna ya kufanya maboresho katika Mfumo wa haki jinai nchini.
“Ndugu washiriki , niwaombe hapa muangalie maeneo yote yanayotoa mwanya kwa maafisa wanaohusika na uzuiaji wa uhalifu, ukamataji wahalifu, uendeshaji mashtaka, utoaji adhabu na urekebishaji wahalifu, vitendo hivi vinafanya wananchi waone kuwa hawatendewi haki na Seriakli yao na hivyo kusababisha wananchi kusigishana na Serikali yao kutokana na vitendo vinavyofanywa na maafisa wa Serikali katika maeneo hayo,” amesema.
Amesema uamuzi wa kuufanyia maboresho mfumo wa haki jinai ili uweze kuendana na nyakati zilizopo utawezesha kila mwananchi kupata haki yake pale anapostahili na hivyo kuondoa dhana ya kuoneana ambayo imeshamiri kwa wananchi.
Amesema anaamini kuwa maboresho katika mfumo huo yatawezesha watendaji katika maeneo husika kuondokana na tabia za mazoea ambazo zimekuwa kawaid kwa watendaji hao kuwaonea wananchi na hivyo kuwanyima haki.
Bw. Sagini pia ametaka washiriki kuangalia namna ya kuboresha maeneo ya uwezeshaji kwa watendaji wa serikali ili kupunguza vitendo mbadala kwa ajili ya kufanikisha utendaji wa kazi zao ikiwa ni pamoja na kuongezwa kwa program za mafunzo zitakazowafanya wahalifu wakiwa gerezani kupata ujuzi na utaalamu wa maeneo fulani na hivyo kuwa raia wema ambao hawako tayari kurejea magerezani pindi wanapokuwa wameachiliwa kutoka huko.
Amesema maeneo hayo yakizingatiwa yataimarisha Imani ya wanachi kwa serikali yao na hivyo kuona wako katika mikono salama huku wakiamini kuwa Serikali yao iko pamoja nao katika kuhakikisha wananchi wote wanapata haki.