Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Michezo ya kubahatisha ya Biko, Charles Mgeta, kulia akizungumza jambo katika uzinduzi wa kibiashara kati ya Biko na Kampuni ya Vodacom kupitia bidhaa ya Mpesa, ambapo wachezaji wa Biko wanaotumia mpesa watakuwa na droo yao mbali na droo za kawaida za Jumapili na Jumatano. Wengine pichani ni Arjuun Dhillon, ambaye ni Mkurugenzi Kitengo cha Biashara kutoka Vodacom na Ali Z Ali Mkuu wa Kitengo Cha uzalishaji cha wateja wakubwa wa Vodacom. Picha na Mpigapicha Wetu
****************
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Kampuni ya mchezo wa kubahatisha wa Biko, wameungana na Kampuni ya Mtandao wa Simu za Mikononi ya Vodacom Tanzania kwa kuhakikisha kwamba wachezaji wa mchezo huo wanaotumia Mpesa kushinda zaidi kwa kuendeshwa droo maalum inayohusisha watumiaji wa Mpesa pekee.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Biko, Charles Mgeta, alisema droo hiyo ni tofauti na zile za kawaida zinazofanyika kila Jumatano na Jumapili kwa watumiaji wa mitandao yote nchini Tanzania, wakiwa na dhamira ya kupanua wigo wa ushindi kwa Watanzania wote, hususan wanaotumia Mpesa.
“Kwa kuendeshwa mchezo huu, sasa wigo wa ushindi umepanuka kutoka mara mbili hadi tatu, kama vile zawadi za papo kwa hapo, zawadi kubwa ya wiki ya Jumatano au jumapili, bila kusahau droo kubwa ya wachezaji pekee wa Mpesa ambao wao pekee watatafutwa mara baada ya kupata washindi wetu wa kawaida kutoka Biko.
“Tunadhani sasa kushinda Biko ni rahisi zaidi, ukizingatia kuwa droo zetu zote zinachagizwa na tumaini letu la kugawa zawadi za juu kwa Watanzania wetu, hivyo ukiacha wigo wa droo zetu za kawaida, bado upo ukumbi muhimu wa watumiaji wa Mpesa ambao wote watacheza kwa mfumo wa kawaida wa kutumia namba yetu ya Kampuni ya 505050 na kumbukumbu namba 2456,”alisema Mgeta.
Naye Mkuu wa Kitengo Cha Uzalishaji Cha wateja wakubwa, Ali Z Ali, aliishukuru Biko kwa kuanzisha droo mahususi kwa ajili ya wateja wao wa Mpesa, akisema kuwa itaonyesha ni namna gani wametambua huduma nzuri kutoka Vodacom Tanzania.
“Vodacom kupitia Mpesa na wenzetu Biko tupo kwa ajili ya wateja wetu wote ambao sasa fursa za ushindi kwao ni pana zaidi, hivyo tunawaasa watumie fursa hii ili wajishindie zawadi kutoka Biko kila siku,”Alisema Ali.
Mbali na droo hiyo maalum ya Biko kwa wateja wa Mpesa, zawadi za papo kwa hapo zinaendelea kutoka kwa wachezaji wa Biko wa mitandao yote ya Tigopesa, Airtel Money, Halopesa na Mpesa, ambapo namba ya Kampuni ni 505050 na kumbukumbu namba 2456, huku zawadi za papo kwa hapo kuanzia sh 5000 hadi milioni moja, bila kusahau droo kubwa za wiki za Jumatano na Jumapili.