Home Mchanganyiko UZINDUZI WA MAONYESHO RUVUMA

UZINDUZI WA MAONYESHO RUVUMA

0

*************

24/07/2019         RUVUMA

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amewataka wamiliki wa viwanda mkoani Ruvuma kuzingatia usalama na afya katika maeneo yao ya kazi.

Akizungumza katika uzinduzi wa maonyesho ya viwanda mkoani Ruvuma, Mndeme amesema wanapozalisha bidhaa mbalimbali lazima wazingatie swala zima la usalama ili kuepukana na majanga ambayo yanaweza kutokea na hivyo kusisitiza elimu ya usalama na afya mahala pakazi kuzingatiwa.

Kwa upande wake mtaalamu wa mazingira kutoka wakala wa usalama na afya mahali pakazi (OSHA) JOSSAM KAMANZA amese ili kufikia malengo na kuimalisha usalama katika mahala pa kazi lazima kuwepo na ushirikiano  baina ya mwajiri na mwajiliwa.

Maonyesho ya viwanda mkoani Ruvuma yamezinduliwa jana tarehe 24 katika kiwanja cha maji maji mjini songea na mkuu wa mkoa huo Christina Mndeme na kilele kitakuwa tarehe 26/07/2019/