Home Mchanganyiko MHE HASUNGA ATETA NA MADEREVA WA MALORI MKOANI SONGWE

MHE HASUNGA ATETA NA MADEREVA WA MALORI MKOANI SONGWE

0

 

Mbunge wa Jimbo la Vwawa mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo mbele ya wanachama wa chama cha Madereva wa Malori mkoani Songwe tarehe 24 Julai 2019 wakati alipokutana nao kwa ajili ya mazungumzo. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Mbunge wa Jimbo la Vwawa mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akikabidhi mchango wake kwa Mwenyekiti wa  Chama cha Madereva wa Malori mkoani Songwe Ndg Deogratius Agripa tarehe 24 Julai 2019.
 Mbunge wa Jimbo la Vwawa mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa chama cha Madereva wa Malori mkoani Songwe tarehe 24 Julai 2019 wakati alipokutana nao kwa ajili ya mazungumzo.
Mbunge wa Jimbo la Vwawa mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo mbele ya wanachama wa chama cha Madereva wa Malori mkoani Songwe tarehe 24 Julai 2019 wakati alipokutana nao kwa ajili ya mazungumzo.
 
Na Mathias Canal, Wizara ya
Kilimo-Songwe
 
Mbunge wa Jimbo la Vwawa
mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga leo tarehe 24 Julai
2019 amekutana na kufanya mazungumzo na madereva wa Malori mkoani Songwe ili
kubaini changamoto zinazowakabili.
 
Katika mkutano huo
uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chama Cha Mapinduzi katika eneo la
Vwawa mkoani Songwe Mhe Hasunga amewahakikishia madereva hao kuwa serikali ya
awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli imejipanga vyema
katika ujenzi wa miundombinu ili kuimarisha usafirishaji.
 
Alisema kuwa serikali
inaendelea na mpango wake wa uboreshaji wa miundombinu zikiwemo barabara kubwa
na ndogo ili kuongeza ufanisi wa magari yanayotumia barabara hizo kumaliza
safari zao katika hali ya usalama.
Kadhalika madereva hao
wamempongeza Mbunge huyo wa Jimbo la Vwawa kwa kuteuliwa na Mhe Rais Dkt John
Pombe Magufuli kuwa waziri katika sekta muhimu ya kilimo hapa nchini kwani
jambo hilo limeongeza heshima.
 
Walisema kuwa imani iliyoonyeshwa
na Rais Magufuli kwa wananchi wa Vwawa na Mkoa wa Songwe kwa ujumla ni matokeo
ya imani ya wananchi hao waliyoionyesha kwa mbunge huyo baada ya kumchagua kwa
kishindo katika uchaguzi mkuu uliofanyika Octoba 2015.
 
Mhe Hasunga ameahidi
kushirikiana na chama hicho cha madereva ili kutatua changamoto zinazowakabili.
 
MWISHO