Wakazi wa Kijiji cha Hanseketwa kilichopo kata ya Ihanda wakimlaki Mbunge wa Jimbo la Vwawa mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga mara baada ya kuwasili katika kijiji hicho akiwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo jimboni humo. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Sehemu ya wakazi wa kijiji cha Shilanga kilichopo kata ya Ihanda wakifatilia mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Vwawa mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo jimboni humo.
Mbunge wa Jimbo la Vwawa mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati akizungumza na Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe Ndg David Kafulila mara baada ya kuwasili mkoani humo kw aajili ya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo jimboni humo.
Sehemu ya wakazi wa kijiji cha Hanseketwa kilichopo kata ya Ihanda wakimsikiliza kwa makini Mbunge wa Jimbo la Vwawa mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo jimboni humo.
Sehemu ya wakazi wa kijiji cha Shilanga kilichopo kata ya Ihanda wakimsikiliza kwa makini Mbunge wa Jimbo la Vwawa mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo jimboni humo.
Na Mathias Canal, Wizara ya
Kilimo-Songwe
Kilimo-Songwe
Mbunge wa Jimbo la Vwawa mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amewahimiza wananchi kujiandikisha kwenye daftari la mkaazi ili kupata fursa ya kuchagua viongozi bora katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Mhe.Hasunga ametoa wito huo leo tarehe 24 Julai 2019 kwa wananchi wakati wa mikutano ya hadhara aliyoifanya katika kijiji cha Ipapa, Ipanzya na Mpela katika kata ya Ipunga sambamba na vijiji vya Maronji, Shilanga na Hanseketwa vilivyopo katika kata ya Ihanda.
Alisema kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa kwa ajili ya kuchagua wajumbe na wenyeviti wa Vitongoji, Vijiji na Mitaa ni muhimu kwani ndio sehemu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu utakaowahusisha Madiwani, Wabunge pamoja na Rais.
Hivyo umuhimu wa wananchi kujiandikisha ni sehemu ya kufanya maamuzi ya viongozi watakaowawakilisha katika kipindi cha miaka mitano kwa ajili ya kuchochea shughuli za maendeleo.
Akizungumzia changamoto zinazowakabili wananchi katika jimbo hilo ambazo kwa sehemu kubwa zimetajwa kuwa ni pamoja na uboreshaji wa barabara, Zahanati na upatikanaji wa maji, Mhe Hasunga alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt .John Pombe Magufuli imejikita katika dhamira ya utatuzi wa changamoto hizo kwa
kipindi cha muda mfupi na malengo ya muda mrefu.
kipindi cha muda mfupi na malengo ya muda mrefu.
Mbele ya wananchi Mhe Hasunga amekiri kuwa kumekuwa na tatizo sugu na la muda mrefu kwenye sekta ya Kilimo la kuchlewa kwa pembejeo kuwafikia wakulima lakini tayari amekemea na kuagiza Taasisi zinazohusika kufikisha pembejeo kwa wakati.
Alisema kuwa Uongozi wa Taasisi itakayoshindwa kufikisha pembejeo kwa wakati na kukwamisha juhudi za serikali katika kuongeza tija na uzalishaji wa mazao ya wakulima utachukuliwa hatua za haraka ikiwemo kusimamishwa kazi.
Kadhalika Mhe Hasunga amepiga marufuku kuzuia kwa kufunga mipaka ya biashara ya Mazao badala yake wananchi wametakiwa kuuza popote watakapo.