Naibu Waziri wa Kilimo, Mh.Hussein Bashe akiongea na Baadhi ya Wadau wa Nafaka hapa nchini pamoja na Balozi wa Kenya nchini Tanzania baada ya kukaa pamoja kuona ninamna gani wanaweza kutatua changamoto ya biashara ya mazao kwa nchi zote mbili
*****************
NA EMMANUEL MBATILO
NAIBU Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, ameagiza kufanyika kikao cha kuondoa urasimu wa biashara ya nafaka kati ya Tanzania na Kenya ili kuwezesha wanayabiashara kufanya kazi hiyo bila usumbufu.
Mh.Bashe alitoa kauli hiyo katika kikao na Balozi wa Kenya nchini,Bw. Dan Kazungu, kilichofanyika Dar es Salaam jana kwa lengo la kuiuzia nchi hiyo mazao ya chakula hasa mahindi.
Akizungumza katika kikao hicho Mh.Bashe aliagiza kushughulikiwa kwa vikwazo vyote vinavyokwamisha usafirishaji wa mazao kwenda Kenya ikiwa ni pamoja na kufanyika utaratibu utakawawezesha mfanyabiashara wanaonunua mahindi kutoka Tanzania kupewa taarifa zitakazowawezesha kusafirisha bila kukaguliwa tena njiani.
Aidha Mh.Bashe alisema kwa sasa kumekuwa na usumbufu mwingi mwa wafanyabiashara wanaosafirisha mahindi kwenda Kenya ambapo wamekuwa wakilazimika kukaguliwa mara kwa mara huku wengine wakikwama mpakani kwa muda mrefu.
Alisema nchini hizo zimekubaliana kuuziana mahindi ambapo Kenya imesema uhitaji wake ni tani tani milioni moja kwa kipindi cha mwaka mmoja, kiasi ambacho bodi ya mazao mchanganyiko imethibitisha kwamba inao uwezo wa kuhudumia.
Pia alisema hategemei mkurugenzi wa bodi ya mazao mchanganyo na ata-behave kama lile shirika la Taifa la Usagishaji ambapo alimtaka kuhakikisha kama wafanyabisahara kutoka Kenya watatuma barua pepe azijibu haraka hata kama ni usiku.
“Balozi wa Kenya atachukua mawasiliano atakuwa anawasiliana na wewe kama mfanyabiashara yeyote anakuwa anahitaji kufanya biashara na sisi” alisema Bashe.