Home Mchanganyiko Jengo la tamisemi lavutia mji wa serikali

Jengo la tamisemi lavutia mji wa serikali

0

****************

Heshima hii inakuja baada ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) kukamilisha jengo lake ambalo kwa hakika ni jengo linalovutia katika mji wa Serikali.

Aprili mwaka huu, Viongozi wa wizara hiyo wakiongozwa na Waziri Selemani Jafo walitekeleza agizo la Rais John Magufuli alililolitoa la kuzitaka Wizara zote kuhamia katika mji huo.

Kutokana na agizo hilo, viongozi hao walihamia na kufanya kazi ya kuwahudumia wananchi ndani ya mabanda ya mabati yaliyokuwapo  kwenye jengo hilo ambayo  yanatumiwa na mkandarasi.

Ikiwa ni miezi minne tangu kufanya kazi zao kwenye mabanda kwasasa wapo ndani ya jengo hilo zuri na la kuvutia.

Ama kwa hakika subira yavuta heri na baada ya dhiki ni faraja, kweli TAMISEMI mmeonesha ubora wenu kwenye matumizi ya mfumo wa Force Account.

Akizungumza leo kuhusu jengo hilo, Waziri huyo amesema siri ya mafanikio ya ujenzi wa jengo hilo zuri ni matumizi ya  Force Account kwa gharama ya Sh.Bilioni moja na imethibitisha kwamba Serikali ya Dk.John Pombe Magufuli inaweka alama zisizofutika.

“Niwapongeze Viongozi na watendaji wote wa OR-TAMISEMI kwa ubunifu ulio tukuka,”amesema 

Ameongezea kuwa Yajayo yanafurahisha kwani siku chache zijazo Jengo lingine Pacha la Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini(TARURA) litaongeza kunogesha Mji wa Serikali.