Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiwa kwenye chumba cha pampu za kusukumia maji za Mradi wa Maji wa Chankorongo katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita, mkoani Geita.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akikagua ujenzi wa tenki la maji la Mradi wa Maji wa Chankorongo katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita, mkoani Geita.
Uchimbaji wa kisima cha maji cha Mradi wa Maji wa Manga ukiendelea wilayani Geita katika mkoa wa Geita.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiwasisitiza wakazi wa Kijiji cha Luhuha kuhusu matumizi ya majisafi na salama yanayotokana na Mradi wa Maji wa Luhuha na kuachana na maji yasiyo salama katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita, mkoani Geita.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akimtua mama ndoo katika Kijiji cha Chigunga, miongoni mwa vijiji vitano vinavyonufaika na Mradi wa Maji wa Chankorongo katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita, mkoani Geita.
………………………
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amesisitiza uwajibikaji kwa watendaji wa Wakala ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) na kusema Wizara ya Maji imewasimamisha Wahandisi wa Maji 67 kwa kushindwa kutimiza majukumu yao kwa weledi na kusababisha ujenzi wa miradi ya maji kukwama.
Lengo la kuwasimamisha kazi wahandisi hao ni kuongeza uwajibikaji kwa wataalam wanaosimamia ujenzi wa miradi ya maji katika maeneo mbalimbali, iweze kuleta tija kwa kufikisha huduma ya maji kwa wananchi.
Mhe. Aweso ametoa ufafanuzi huo wakati akiwa ziarani katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita, mkoani Geita mara baada ya kukagua ujenzi wa Mradi wa Maji wa Chankorongo uliogharimu kiasi cha Shilingi bilioni 4.9 na kuhudumia vijiji vya Chankorongo, Chigunga, Nyakafulo, Kabugozo na Chikobe vilivyopo katika Kata ya Busanda.
‘‘Naamini Wakala ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) itakuwa suluhisho la tatizo la utekelezaji wa miradi ya maji vijijini kwa sababu tumewasimamisha kazi wahandisi 67 na kubaki na wahandisi wazuri na wenye uwezo wa kutekeleza majukumu yao kwa weledi’’, Aweso amesema.
‘‘Kupitia RUWASA tutaleta mapinduzi makubwa vijijini kuanzia hatua ya usanifu, ujenzi na usimamizi wa miradi kutokana na mabadiliko makubwa ya mfumo, ambapo awali ulikuwa kikwazo kwa miradi ya maji vijijini kufanikiwa’’, Aweso amesema.
Vilevile, Mhe. Aweso amekagua miradi ya maji ya Manga, Kasamwa na Bulela katika Mji wa Geita akiwataka wahandasi wa maji kutimiza wajibu wao na kufanikisha azma ya Mhe. Rais Magufuli ya Kumtua Mama Ndoo Kichwani.
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Aweso ametoa rai yake kwa wananchi kuchangia huduma ya ya maji ili miradi iweze kujiendesha kwa mafanikio na kudumu kwa muda mrefu, ikiwemo kuwa waaminifu na fedha zinazotokana na makusanyo yanayotokana na mauzo ya maji.
Akisisitiza fedha hizo ni lazima ziwe na utaratibu mzuri wa mapato na matumizi kwa kamati za maji, kinyume na hapo miradi iliyogharimu Serikali fedha nyingi za ujenzi haitakuwa msaada kwa wananchi.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiwa kwenye chumba cha pampu za kusukumia maji za Mradi wa Maji wa Chankorongo katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita, mkoani Geita.Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akikagua ujenzi wa tenki la maji la Mradi wa Maji wa Chankorongo katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita, mkoani Geita.Uchimbaji wa kisima cha maji cha Mradi wa Maji wa Manga ukiendelea wilayani Geita katika mkoa wa Geita.Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiwasisitiza wakazi wa Kijiji cha Luhuha kuhusu matumizi ya majisafi na salama yanayotokana na Mradi wa Maji wa Luhuha na kuachana na maji yasiyo salama katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita, mkoani Geita.Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akimtua mama ndoo katika Kijiji cha Chigunga, miongoni mwa vijiji vitano vinavyonufaika na Mradi wa Maji wa Chankorongo katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita, mkoani Geita.………………………Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amesisitiza uwajibikaji kwa watendaji wa Wakala ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) na kusema Wizara ya Maji imewasimamisha Wahandisi wa Maji 67 kwa kushindwa kutimiza majukumu yao kwa weledi na kusababisha ujenzi wa miradi ya maji kukwama.Lengo la kuwasimamisha kazi wahandisi hao ni kuongeza uwajibikaji kwa wataalam wanaosimamia ujenzi wa miradi ya maji katika maeneo mbalimbali, iweze kuleta tija kwa kufikisha huduma ya maji kwa wananchi.Mhe. Aweso ametoa ufafanuzi huo wakati akiwa ziarani katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita, mkoani Geita mara baada ya kukagua ujenzi wa Mradi wa Maji wa Chankorongo uliogharimu kiasi cha Shilingi bilioni 4.9 na kuhudumia vijiji vya Chankorongo, Chigunga, Nyakafulo, Kabugozo na Chikobe vilivyopo katika Kata ya Busanda. ‘‘Naamini Wakala ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) itakuwa suluhisho la tatizo la utekelezaji wa miradi ya maji vijijini kwa sababu tumewasimamisha kazi wahandisi 67 na kubaki na wahandisi wazuri na wenye uwezo wa kutekeleza majukumu yao kwa weledi’’, Aweso amesema.‘‘Kupitia RUWASA tutaleta mapinduzi makubwa vijijini kuanzia hatua ya usanifu, ujenzi na usimamizi wa miradi kutokana na mabadiliko makubwa ya mfumo, ambapo awali ulikuwa kikwazo kwa miradi ya maji vijijini kufanikiwa’’, Aweso amesema.Vilevile, Mhe. Aweso amekagua miradi ya maji ya Manga, Kasamwa na Bulela katika Mji wa Geita akiwataka wahandasi wa maji kutimiza wajibu wao na kufanikisha azma ya Mhe. Rais Magufuli ya Kumtua Mama Ndoo Kichwani.Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Aweso ametoa rai yake kwa wananchi kuchangia huduma ya ya maji ili miradi iweze kujiendesha kwa mafanikio na kudumu kwa muda mrefu, ikiwemo kuwa waaminifu na fedha zinazotokana na makusanyo yanayotokana na mauzo ya maji.Akisisitiza fedha hizo ni lazima ziwe na utaratibu mzuri wa mapato na matumizi kwa kamati za maji, kinyume na hapo miradi iliyogharimu Serikali fedha nyingi za ujenzi haitakuwa msaada kwa wananchi.