Mbunge wa jimbo la Kigamboni Mhe.Faustine Ndugulile ameendelea na ziara yake mtaa kwa mtaa katika kata ya Kisarawe II kwa kutembelea mitaa ya Madege, Sharifu na Kichangani katika Kata ya Kisarawe II na kuongea na wananchi kwa lengo la kusikiliza kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili katika maeneo yao.
Mbunge wa jimbo la Kigamboni Mhe.Faustine Ndugulile ameendelea na ziara yake mtaa kwa mtaa katika kata ya Kisarawe II kwa kutembelea mitaa ya Madege, Sharifu na Kichangani katika Kata ya Kisarawe II na kuongea na wananchi kwa lengo la kusikiliza kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili katika maeneo yao.Katika ziara hii, Mhe Ndugulile aliwaeleza Wananchi hao kuhusu jitihada mbalimbali za kimaendeleo zilizozifanyika Jimboni.Aidha Mhe.Ndugulile amewezesha kupatikana kwa Tsh Milioni 75 kwa ajili ya ujenzi wa Mabweni ya sekondari ya Kisarawe II na Milioni 90 kwa ajili ya ujenzi wa Maktaba na Madarasa.Hata hivyo Mhe.Ndugulile ameweza pia kufanikiwa kupatikana kwa kompyuta 10 zenye thamani ya Tsh millioni 15 kwa ajili ya Masomo ya Tehama katika shule hiyo. Lengo ni kuifanya Sekondari iwe na kidato cha tano na sita ifikapo mwaka 2020.DKT. Ndugulile aliipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kwa kutenga zaidi Tsh 380,000,000 kwa miradi mbalimbali ya maendeleo.Dkt Ndugulile alimshukuru Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kulipatia Jimbo la Kigamboni kiasi cha Tsh Billioni 90 ya ujenzi wa barabara za Kigamboni ikiwa ni pamoja na Barabara ya Kibada-Mwasonga-Kimbiji.Dkt.Ndugulile alitumia mkutano kuhamasisha wana Kigamboni kujiandaa na chaguzi za Serikali za Mitaa kwa kuajindikisha kupiga kura pindi daftari la kupiga kura litakapofika Kigamboni na pia amewataka wananchi kujisajili kwa lengo la kupata vitambulisho vya uraia.Dkt.Ndugulile atandelea na zaiara yake leo katika kata ya kibada