Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro ameungana na Mhe Mbunge Dkt. John Danielson Pallangyo wa Arumeru Mashariki pamoja na mwenyekiti wa Bodi ya shule ya kata ya Kisimiri Ndugu Elishilia Kaaya Shule ambayo imefanya vizuri kitaifa katika matokeo ya kidato cha sita Kwa kuwashukuru kwa kuwafanyia Mambo makubwa mawili la kwanza kutoa eneo lenye hekari 7 kwa ajili ya mradi wa walimu wa Kisimiri City pamoja na kuwapatia fedha Mkuu wa shule tumempatia kiwanja cha kujenga nyumba kama sehemu ya motisha ya kazi nzuri wanayofanya
Ndugu Muro amesema wiki ijayo wataelekea katika shule ingine ya Mwandeti iliyopo wilaya ya Arumeru ambayo nayo imekuwa ya Nne kitaifa kuwashukuru walimu waliosaidia shule hiyo kufanya vizuri