Mkuu wa shule ya Kibaha Sekondari Chrisdom Ambilikile akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake kuhusiana na mikakati mbali mbali aliyojiwekea katika kuhakikisha anapandisha zaidi kiwango cha elimu, pamoja na mpango wa kufanya harambee kubwa ya kuwakutanisha viongozi wa serikali na wabunge waliosomea katika shule hiyo ili kuzitatua changamoto zilizopo katika sekta ya ellimu.(PICHA NA VICTOR MASANGU).
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha sita wanaosoma katika shule ya Kibaha sekondari mkoani Pwani wakiwa darasani wakiendelea na masomo yao ya kawaida kwa ajili ya kujiandaa na mitihani yao mbali mbali ya majaribio na ule wa Taifa.
Mkuu wa shule ya Kibaha Sekondari Chrisdom Ambilikile akiwaonyesha baadhi ya waandishi wa habari hawapo pichani chumba cha maabara ambacho kimefanyiwa ukarabati na serikali kwa lengo la kuweza kuwapa fursa wanafunzi kujifunza zaidi kwa vitendo.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
Kaka mkuu wa serikali ya wanafunzi wa shule ya Kibaha Sekondari Jonasi Baraka akizungumzia changamoto mbali mbali zinazowakabili katika shule hiyo pamoja na mipango waliyojiwekea katika kuongeza kiwango cha ufaulu katika matokeo yajayo ya kidato cha sita.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
Mmoja wa wajumbe wa kamati ya wazazi ya maendeleo katika shule ya Kibaha Sekondari Dk. Hamisi Likuli akifafanua jambo kuhusiana na hatua mbali mbali ambazo tayari wameshazichukua katika kuhakikisha wanashirikiana na serikali ya awamu ya tano katika kuboresha sekta ya elimu katika shule hiyo.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU).
VICTOR MASANGU, PWANI
SHULE kongwe ya wavulana ya vipaji maalumu ya Kibaha sekondari iliyopo Mkoani Pwani licha ya kushika nafasi ya kwa kitaifa katika matokeo ya kidato cha sita kwa mwaka wa 2018 na kushika nafasi ya sita kwa mwaka 2019 bado wanafunzi wake kwa sasa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa walimu ya masomo ya sayansi,uhaba wa vitabu, uchakavu wa miundombinu ya madarasa,uhaba wa vitanda pamoja na upungufu wa matundu ya vyoo.
Hayo yamebaishwa na baadhi ya wanafunzi hao akiwemo Jonasi Baraka ambaye ni kaka mkuu wa serikali ya wanafunzi wa shule hiyo pamoja na Kalani Mahila ambapo wamedai kuwa serikali ya awamu ya tano inapaswa kulivalia njuga suala hilo kwa kuharakisha kufanya ukarabati wa majengo hayo ambayo yanaweza kuhatarisha usalama wa maisha yao.
Aidha wanafunzi hao wamesema kwamba lengo kubwa ni kuhakikisha wanasoma katika mazingira rafiki ambayo yatawafanya waongeze kiwango cha ufaulu hivyo
wameiomba serikali ya awamu ya tano kuwakarabatia majengo ..vyoo vinavyotumika kwa sasa ni vinne tu, kwa idadi ya wanafunzi ..vyoo vingine vimefungwa kutokana na ubovu ..maabara na walimu wa masomo ya sayansi
“Kwa sasa kwa kweli shule yetu ya Kibaha tunakabiliwa na changamoto mbali mbali lakini kitu kikubwa tunachohitaji kutoka kwa serikali yaawamu ya tano ni kutuboreshea sekta ya elimu kwa kutufanyia ukarabati wa miundombinu ya majengo mbali mbali yakiwemo ya madarasani, vyoo, pamoja na mabweni ambayo kwa hali yake kwa sasa sio nzuri yamechakaa, na sisis nia yetu ni kushika nafasi ya kwanza kitaifa,”walisema wanafunzi hao.
Naye mmoja wa wajumbe wa kamati ya wazazi ya maendeleo katika shule ya Kibaha Sekondari Dk. Hamisi Likuli amekiri kuwepo kwa changamoto mbali mbali zinazowakabili wanafunzi hao,ambapo alibainisha hatua ambazo tayari wameshazichukua ni kuimarisha huduma ya afya, kuboresha miundombinu ya majengo na vyoo ,kujenga uzio pamoja na upatikanaji ya huduma ya maji kwa kuweka matanki pamoja na kuchimba kisima.
Katika kukabiliana na changamoto hizo Mkuu wa shule hiyo ya Kibaha Chrisdom Ambilikile ameamua kuja na mpango wa kuwakutanisha viongozi mbali mbali wa serikali pamoja,wabunge pamoja na wadau wengine ambao wamesomea katika shule hiyo kwa dhumuni la kufanya harambee ambayo inanatajia kufanyia Septemba 9 mwaka huu lengo ikiwa ni kusaidia kutatua changamoto ambazo zinaikabili shule hiyo kwa kipindi cha miaka mingi.
Mkuu huyo alibainisha kuwa licha ya shule yake kushika nafasi ya sita kwa mwaka huu katika matokeo ya kidato cha sita kitaifa lakini kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi kimeongezeka kwa daraja la kwanza kuwa na wanafunzi wapatao 143 waliopata divisheni 1.
“Kwa kweli ukizungumzia kitaalamu utaona sisi shule yetu kwa matokeo ya kidato cha sita kwa mwaka huu wa 2019 tumeshika nafasi ya sita kitaifa lakini mwaka jana tulishika nafasi ya kwanza lakini kiwango cha daraja la kwanza kimeongezea sana tumepata wanafunzi 143 kwa hivyo utaona tumefanya vizuri na kuwa na nafasi kubwa ya kuwapeleka wanafunzi wengi vyuoni,”alisema Mkuu huyo.
Pia mikakati yetu tuliyojiwekea ni kushirikiana bega kwa began a wazazi, pamoja na wadau wa maendeleo katika kuiboresha shule hiyo ambayo wanatarajia kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 1.6 kwa ajili ya mradi mkubwa wa ujenzi wa jengo kubwa la kisasa ambalo litakuwa likitumika kwa matumizi mbali ikiwemo maktaba,kompyuta pamoja na mambo mengine yanayohusiana na elimu.
Shule hiyo kongwe ya Kibaha sekondari yanye wanafunzi 669 na walimu 56 ilianzishwa mwaka 1965 ambapo viongozi mbali mbali wa serikali na wabunge wameweza kusomea hapo akiwemo Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Spika wa Bunge Goroge Ndugai sambamba na Free Man Mbowe Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) pamoja na Razaro Nyarandu.