*******************
Serikali imetoa fursa kwa wawekezaji kujenga viwanda vya dawa pamoja na vifaa tiba hapa nchini ili kuwepo kwa uwezekano wa wa hupatikanaji wa dawa pamoja na vifaa tiba hapa nchini pasipokuagiza nje ya nchi.
Ameyasema hayo leo Waziri wa Biashara na Viwanda Mheshimiwa Innocent Bashungwa katika kikao ambacho kiliwakutanisha Taasisi ya bohari ya Dawa (MSD) pamoja na wawekezaji mbalimbali kutoka hapa nchini na nje ya nchi.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Bw.Laurean Bwanakunu takwimu za uhakika za 2016(Tanzania Local Pharma Strategey Paper) soko la mahitaji ya Dawa, vifaa Tiba na Vitendanishi vya maabara Tanzania lilifikia 457 milioni za marekani kwa mwaka, ambazo ni sawa na karibu shilingi trilioni moja za kitanzania kwa mwaka.
Bw.Bwanakunu amesema kuwa uhakika ulio wazi ni kwamba Zaidi ya asilimia 85 ya kiasi hicho cha pesa kutoka nchi hutumika kuagiza mahitaji ya dawa na vifaa tiba kutoka nje ya nchi.
“Ili kupunguza utegemezi huu mkubwa wa dawa na vifaa tiba kutoka mataifa ya nje,MSD imeibua wazo jipya la kuanzisha viwanda vya kuzalisha dawa na vifaa tiba hapa nchini kwa kushirikiana na sekta binafsi, yaani Public Private Partnership (PPP). Amesema Bw.Bwanakunu.
Pamoja na hayo Bw.Bwanakunu amesema kuwa katika kutekeleza wazo hilo,MSD ilimuajili mshauri mwelekezi ili kufanya upembuzi yakinifu ambao umeonesha matokeo chanya yenye manufaa makubwa kwa serikali na wawekezaji husika.
Aidha Bw.Bwanakunu amesema kuwa katika uanzishaji viwanda hivyo imeshauriwa kuwa kiwanda cha bidhaa za hospitali za pamba kijengwe mkoani Mwanza, Kiwanda cha maji-tiba kijengwe mkoani Mbeya na kasha kiwanda cha cha dawa mchanganyiko (General Pharma kijengwe Mkoani Pwani.