Home Mchanganyiko DC KOROGWE AUNGANA NA WANANCHI KUSHUHUDIA MAJARIBIO YA TRENI YA MIZIGO RELI...

DC KOROGWE AUNGANA NA WANANCHI KUSHUHUDIA MAJARIBIO YA TRENI YA MIZIGO RELI YA TANGA-MOSHI.

0

 

Ikiwa zimebaki siku chache kuelekea katika sherehe za ufunguzi wa Reli ya kutoka Tanga kwenda Kilimanjaro, Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mh Kissa Kasongwa akiwa katika mkutano na wananchi wa Kata ya Magila gereza amelazimika kusimamisha mkutano na kushuhudia majaribio ya Treni ya mizigo iliyokuwa ikifanya safari zake katika reli ya kutoka Tanga kwenda Kilimanjaro ambayo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi ifikapo julai 20-2019 wilayani Moshi.

Dc Kissa amesema kuwa ni bahati kubwa kwa wanakorogwe kuhushudia majaribio hayo ya Treni ya mizigo ikifanya safari katika reli ambayo inapita wilayani Korogwe ikitokea Tanga na kwamba nao wameshiriki kwa namna moja au nyingine katika shagwe za sherehe hizo za uzinduzi ambapo ni utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi kwa maana iliahidi na sasa imetekeleza.

Kufunguliwa kwa Reli hii ya kupitisha treni za mizigo kutoka Tanga kwenda Kilimanjaro kutasaidia sana kukuza uchumi katika mikoa hii miwili inayounganishwa na reli pamoja na Taifa kwa ujumla.