Rose Joseph Afisa mawasiliano Mwandamizi Chuo Kikuu cha Muzumbe akiwapa maelezo namna unavyoweza kujiunga na chuo hicho na kozi mbalimbali zinazotolewa chuoni hapo wananchi mbalimbali wamekuwa wakitembelea banda la Mzumbe katika maonesho ya vyuo Vikuu yanayofanyika Mnazi mmoja jijini Dar es salaam , Maonesho hayo yanatarajiwa kufunguliwa leo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Kassim Majaliwa.
Maonesho hayo huandaliwa kila mwaka na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania TCU na vyuo vikuu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania vinashiriki katika maonesho hayo.
(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWEBLOG-DAR ES SALAAM)
Baadhi ya maofisa wa Chuo Kikuu cha Mzumbe wakitoa huduma mbalimbali kwa wanafunzi waliotembelea katika banda lao kwenye maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Kelvin Mwita Mhadhiri wa chuo Kkuu cha Mzumbe na John Tropick katikati Afisa Udahili Chuo Kikuu cha Mzumbe wakiwasikiliza baadhi ya wanafunzi na wananchi wanaotaka kujiunga na chuo hicho waliofika katika banda hilo ili kupata maelezo ya msingi kabla ya kufanya maombi ya kujiunga na chuo cha Mzumbe.
Picha mbalimbali zikionesha wananchi wakipata maelezo katika banda la Chuo Kikuu cha Mzumbe.
Bi. Fatna Mfalingundi Afisa Mawasiliano Chuo Kikuu cha Mzumbe akiwapa vipeperushi na kutoa maelezo kwa baadhi ya vijana waliofika katika banda la chuo hicho ilikujionea kozi mbalimbali zitolewazo chuoni hapo.
Picha mbalimbali zikionesha baadhi ya wananchi wenye sifa za kujiunga na Chuo Kikuu cha Mzumbe wakijisajili ili kujiunga na chuo hicho katika maonesho ya vyuo vikuu yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.