*****************
Na Emmanuel Mbatilo
MSANII wa kizazi kipya hapa nchini Bensoni Wiliam maalufu Bensoni wa hauzimi jana aliweza kumzika mwanae kipenzi ambaye umauti ulimfika hivi karibuni baada ya mkewe kujifungua kabla ya muda na kuwa katika uangalizi wa madaktari mpaka umauti ulivyomfika.
Benson na mkewe ambaye alikuwepo katika video ya Hauzimi mpaka sasa wamekuwa pamoja kwa takribani miaka saba na kufanikiwa kupata mtoto mmoja ambaye amefariki hapo jana.
Msanii huyo ametoa shukrani kwa msanii wa filamu hapa nchini Rose Ndauka pia na watu wote ambao walikuwa pamoja katika wakati mgumu ambao anapitia.