Bi. Sylivia Siriwa akiongea na wajumbe wa kikao kazi kuhusu mfumo maalum wa mtandao utakaowezesha kupata wasifu wa wanawake wasomi, wanasiasa na wale wanaofanya kazi za kitaalam nje ya nchi.
Mkurugenzi Mkuu toka TGNP Mtandao Bi. Lilian Liundi akiongea na wajumbe wa kikao kazi kuhusu mfumo maalum wa mtandao utakaowezesha kupata wasifu wa wanawake wasomi, wanasiasa na wale wanaofanya kazi za kitaalam nje ya nchi.
Baadhi ya Washirikiwa kikao kazi kuhusu mfumo maalum wa mtandao utakaowezesha kupata wasifu wa wanawake wasomi, wanasiasa na wale wanaofanya kazi za kitaalam nje ya nchi wakifuatalia mada kuhusu namna mfumo huo utakavyokuwa ukifanya kazi.
Bi. Jennifer Mwengwatoka TGNP Mtandaoakiongea na wajumbe wa kikao kazi kuhusu mfumo maalum wa mtandao utakaowezesha kupata wasifu wa wanawake wasomi, wanasiasa na wale wanaofanya kazi za kitaalam nje ya nchi.
……………………
Na Mwandishi wetu Morogoro.
Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii kwa kushirikiana na TGNP Mtandao inatayarisha mfumo maalum wa mtandao utakaowezesha kupata wasifu wa wanawake wasomi, wanasiasa na wale wanaofanya kazi za kitaalam nje kwa kuweka taarifa zao kwenye mfumo ili iwe rahisi kwao kupata fursa za ajira ikiwemo na uteuzi katika nafasi mbalimbali.
Akiongea wakati wa mapitio ya mfumo huo mapema leo mjini Morogoro Afisa Maendeleo Mkuu kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Sylivia Siriwa amewaambia wajumbe wa Mkutano huo kuwa lengo la Mfumo huo nikuwezesha wanawake wenye vipaji, ubunifu na elimu kuweza kufahamika wapi walipo na kutumia taarifa binafsi au wasifu wao kama taarifa muhimu ya kuwangaunisha na fursa mbalimbali zilizopo na katika uteuzi wa nafasi za uongozi na kutoa maamuzi.
Aidha Bi. Siriwa aliongeza kuwa mfumo huu utasaidia mwajiri na wenye kuhitaji kuajiri mwanamke mwenye sifa, uzoefu na taaluma anayotaka kutumia mfumo huu kumpata kwa kuwa unakuwa na wasifu na taarifa za mhusika tofauti na sasa ambapo waajiri wanakuwa hawana taarifa za wanawake wenye sifa zinazohitajika kukidhi sifa zinazotakiwa na mwajiri.
Naye Mkurugenzi wa TGNP Mtandao Bi. Lilian Liundi aliwambia wajumbe wa kikao kazi hao kuwa baada ya kuanza kutumika na kuweka taarifa za wanawake kwenye mfumo huo ndipo wataweza kuona mapungufu yaliyopo na kuyafanyia kazi ikiwemo kutoa ushauri kwa vyombo vya maamuzi na kuwezesha wanawake pia kuwa katika sehemu za maamuzi na nafasi nyinginezo.
Aidha Bi. Liundi aliongeza kuwa ukienda katika Taasisi binafsi kama Azam na Makampuni ya Mo Enterprises unakuta wanawake ni wachache lakini pengine wamiliki wa kampuni hizo hawana taarifa za uwepo wanawake wenye ujuzi hivyo mifumo kama hii itawezesha wamiliki wa makapuni haya kutoa nafasi kwa wanawake zaidi katika sekta binafsi.
Bi. Liundi aliongeza kuwa pamoja na mfumo huu kuwepo Taasisi yake pamoja na Wizara watafanya uchambuzi wa bodi mbalimbali kuangalia uwiano wa kijinsia kwa kuangalia idadi ya wanawake na wanaume na kutoa ushauri kwa mamlaka za uteuzi kwa kuwasilisha taarifa za wanawake wenye sifa ili kuona kama wanawake wanaweza kuwa sehemu uteuzi wa nafasi zinazotakiwa kulingana na sifa.
Aidha Bi. Liundi alisema kuwa wakati wa uwekaji taarifa katika Mfumo huo wataweza kuona viwango vya wanawake akiwataja kuwa wa viwango vya chini kati na juu jambo litakalo wawezesha kufanya uchambuzi wa namna ya kusaidia kuwainua kiutendaji na kitaaluma kwa wale walio na elimu ya chini kuwapatia fursa za masomo na wale wakati wenye elimu kuwapatia fursa za juu zaidi.
Kuanzishwa kwa mfumo huu kunatokana na azimio la Siku ya Kimataifa ya Wanawake ya mwaka 2017 ambapo Waziri wa Afya Ummy Mwalimu aliagiza kuanzishwa kwa mfumo huu utakaowezesha kuwepo kwa taarifa za wazi kwa wanawake wenye sifa ili waweze kupatikana na kutumiwa kwa Maendeleo ya Taifa.