Timu ya wataalamu wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi wakijadiliana jambo katika moja ya maeneo yanayopendekezwa kuwa Dampo katika Halmashauri hiyo.
Wataalamu wa Halmashauri ya Mbozi wakiangalia bwawa la maji ya mvua pamoja na chemichemi linalotokana na kuchimbwa kwa tabaka la juu la mwamba wa kokoto ambao ulitumika kwenye ujenzi wa barabara miaka ya 80.
Mwananchi huyu akiendesha shughuli za uchimbaji kokoto kwenye Mlima Mbozi, eneo linalopendekezwa kuwekwa Dampo la taka zinazozalishwa katika Miji ya Vwawa na Mlowo.
Bwawa la Mbozi lililopo katikati ya mwamba wa jiwe linaloendelea kutumika kutengeneza kokote kwaajili ya miradi ya Barabara kwenye mkoa wa Songwe. Wananchi wanatumia fursa ya bwawa hilo kufanya shughuli za uvuvi na unyweshaji wa mifugo.
……………………
Na Danny Tweve Mbozi
Timu ya wataalamu wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi wamefanya ukaguzi wa maeneo kadhaa kwaajili ili kutambua eneo linalofaa kuhamishia dampo la taka baada ya lililokuwepo kuwa eneo la mji kutokana na kasi ya ukuaji wa mji wa Vwawa inayotokana na kuwepo kwa makao makuu ya mkoa.
Maeneo kadhaa yaliyobainishwa kwenye mapendekezo yametembelewa na wataalamu na hatimaye mapendekezo yake kuwasilishwa kwenye mamlaka za juu za Halmashauri kwa maamuzi.
Miongoni mwa maeneo hayo ni eneo la mlima Mbozi na Karasha ambayo kwa pamoja yalibainishwa na timu hiyo huku yakitolewa ushauri kulingana na athari za maingira zilizopo kwa kila eneo. Kasi ya ukuaji miji inayoenda sambamba na uzalishaji taka mijini ni moja ya changamoto kubwa zinazozikabili mamlaka za serikali za mitaa ambazo ndiyo zinazopanga maeneo hayo.
Hata hivyo changamoto ya vifaa vya usafirishaji taka na mitambo ya kuhifadhia, ni miongoni mwa maeneo ambayo bado hayajapatiwa ufumbuzi hasa hapa nchini licha ya maeneo machache ya miji kufanikiwa kununua vifaa hivyo.
Mbozi ni moja ya maeneo yenye uhaba wa magari ya kuzolea taka na hata vifaa vya kuhifadhia na katika kutambua hilo.
“mkakati wa halmashauri ni kutafuta wadau itakaoshirikiana nao hasa katika kuzirejesha taka kwaajili ya matumizi (recycling and re-use) ambapo baadhi ya bidhaa kama mbolea, mazuria na mapambo yanaweza kutengezwa kupitia taka” anadokeza mkurugenzi wake Bi Halima Mpita.