Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akiongozana na Spika wa Bunge la Kenya, Mhe. Justin Muturi baada ya kumpokea leo katika uwanja wa ndege wa Jijini Dodoma. Spika Muturi pia ni Mwenyekiti wa kamati tendaji ya Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika, wageni wengine ni wajumbe wa jumuiya hiyo.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akizungumza na Spika wa Bunge la Kenya, Mhe. Justin Muturi katika Ofisi za uwanja wa ndege leo Jijini Dodoma. Kushoto ni katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati), Spika wa Bunge la Kenya, Mhe. Justin Muturi (kulia kwa Spika Ndugai) ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati tendaji ya Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Ndg. Godwin Kunambi wakimsikiliza Mchumi, Mratibu wa dawati la uwekezaji halmashauri ya Jiji la Dodoma, Ndg. Abeid Msangi wakati walipotembelea eneo lao (Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika)
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wanne kushoto), Spika wa Bunge la Kenya, Mhe. Justin Muturi (wa tatu kushoto) ambae pia ni Mwenyekiti wa kamati tendaji ya Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika,wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Mabunge Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika Bungeni Jijini Dodoma. Wa pili kulia ni Katibu wa Bunge la Tanzania na Katibu wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika, Ndg. Stephen Kagaigai
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati), Spika wa Bunge la Kenya, Mhe. Justin Muturi (kulia) ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati tendaji ya Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika wakiingia katika ukumbi wa Bunge la Tanzania wakati wa ziara yao walipotembelea Bunge hilo leo Jijini Dodoma. Wageni wengine ni wajumbe wa Mabunge Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akiagana na Spika wa Bunge la Kenya, Mhe. Justin Muturi katika uwanja wa ndege Jijini Dodoma. Spika Muturi ni Mwenyekiti wa kamati tendaji ya Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika amabe aliongoza ujumbe wa jumuiya hiyo katika ziara ya kikazi ya siku moja Jijini Dodoma.