Home Mchanganyiko CGP PHAUSTINE KASIKE AKAGUA SHAMBA LA MIFUGO GEREZA RUSUMO, AWATAKA KUONGEZA UZALISHAJI...

CGP PHAUSTINE KASIKE AKAGUA SHAMBA LA MIFUGO GEREZA RUSUMO, AWATAKA KUONGEZA UZALISHAJI WA MIFUGO

0

1.Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike (wa tatu toka kulia)
akimsikiliza Mkuu wa Gereza Rusumo, Mrakibu wa Msaidizi wa Magereza,Jackson
Murya alipofanya ukaguzi wa shamba la mifugo katika gereza hilo. Kamishna Jenerali Kasike jana Julai 12, 2019 amewataka Wakuu wote wa Magereza yenye mashamba yenye mifugo nchini kuongeza uzalishaji wa mifugo.

Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike( wa pili toka kushoto) akitoa
maelekezo kwa Watendaji wote katika Gereza la Mifugo Rusumo alipotembelea katika ziara yake ya kikazi jana Julai 12, 2019.

Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Ngara, Mrakibu wa Magereza, Phaustine Makonge
(kushoto) akitoa taarifa ya utendaji ya Gereza kwa Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike alipowasili Gerezani hapo jana Julai 12, 2019.

Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike (katikati) akiwa katika picha
ya pamoja na Maafisa na Askari wa Gereza la Mifugo la Rusumo jana Julai 12, 2019. Wa pili toka kulia aliyeketi ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kagera, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Raymond Mwampashe(Picha zote na Jeshi la Magereza).