Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk Zainab Chaula akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Muongozo wa kozi Huduma za Magonjwa ya Dharura na ajali ambazo zitakuwa msaada mkubwa kupata wataalamu wa kutoa huduma hizo Helen Mtui, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano na viongozi wa MUHAS wakishuhudia tukio hilo.
Viongozi mbalimbali wakipiga makofi mara baada ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Zainab Chaula kuzindua Muongozo wa kozi za Magonjwa ya Dharura na ajali.
………………………………………………………
KATIBU Mkuu wa wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsi Wazee na Watoto Dk. Zainab Chaula, amesema serikali inampango wa kusambaza huduma ya tiba za dharuara,uokoaji na usafirishaji wa majeruhi wa ajali na wagojwa nchini ili kuokoa maisha ya watu wanaopata ajali.
Amesema hayo wakati wa kufunga mafunzo ya watoa huduma wa tiba za dharuara na uzinduzi wa mwongozo wa huduma za dharura ambao unawahitimu wapatao 519 kutoka katika idara mbalimbali katika Chuo kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) jana jijini Dar es salaam.
Dk.Chaula alisema kwa sasa takwimu zinaonesha kuwa kunaongezeka za ajali hivyo mafunzo hayo yatasaidi kufika sehemu za ajali na kuhudumia majeruhi kwa haraka zaidi .
“Lengo la mradi huu ni kueneza kwa nchi nzima mpango hasa ni kila Mtanzania atakapopata ajali au dharura ya afya aweze kuhudumiwa kwa haraka zaidi hii itasaidia kuokoa maisha ya watu wanaopata dharura.
“Pia mradi huu ni sehemu ya uboreshaji wa huduma za afya hapa nchini kwani kazi zitafanywa na wahudumu wa afya wakisaidiana na idara zingine,”alieleza Dk.Chaula.
Hata hivyo Dk Chaula aliwataka wahitimu wa mafunzo hayo kuwa hudumia wananchi bila ubaguzi na kufanya kazi kwa weledi na upendo kwani wagonjwa wanahitaji upendo.
“Kazi hii haiwezi kuwa ngumu kwasababu mmesomea,wahudumieni wananchi bila kujali dini,kabila wala Mkoa alipotoka kazi hii inahitaji upendo hivyo mgonjwa akija anamaumivu msaidi kwa upendo,”alisema Dk .Chaula.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo cha (MUHAS) Dk.Andrea Pembe alisema chuo kinaendelea kuandaa mtaala wa mafunzo ya muda mfupi ya kuhudumia wagonjwa wa dharura na ajali.
Alisema mpaka sasa vituo vilivyowekwa kwaajili ya huduma hiyo ni Tumbi,Kimara, hospitali Morogoro,Ruaha,Temeke,Kinondoni, Ilala,Chalinze,Kigamboni na wataendelea kupeleka wataalamu maeneo mengi.
“Matarajio yetu ni kufikia uchumi wa kati na bila afya njema haiwezekani Hata hivyo chuo kinaandaa mtaala wa mafunzo ya muda mfupi na kuwa tunafanya hivi mara kwa mara ili kuhakikisha utoaji huduma nje ya hospitali unafanikiwa nchi nzima,”alisema Dk.Pembe.
Dk Pembe aliishukuru benki ya dunia na wadau wengine kwa kuwa mstari wa mbele kufanikisha huduma hiyo.
“Tunashirikiana na Jeshi la Wananchi,Jeshi la polisi,Jeshi la zimamoto na uokoaji, shirika la msalaba mwekumndu katika kufanikisha uokoaji wa dharura na pia nashukuru benki ya Dunia kwa kuwa mstari wa mbele kufanikisha hili.
Naye mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo Dk.Hendry Sawe alisema changamoto walizoukutana nazo ni kukwama kupata vifaa kwa wakati na kuchelewa kwa magari ya kubeba wagonjwa.
“Changamoto ni kupata vifaa vya kazi tunaazima kutoka maeneo mengine na pia magari ya kubeba wagonjwa yamekuwa machache na hayafiki kwa wakati,”alisema Dk Sawe.
Dr.Juma Mfinanga Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Dharura na ajali Hospitali ya taifa ya Muhimbili akizungumza wakati wa kutuniku vyeti vya wahitimu wa kozi za huduma ya tiba za dharuara,uokoaji na usafirishaji wa majeruhi wa ajali na wagojwa nchini ili kuokoa maisha ya watu wanaopata ajali katika hafla iliyofanyika MUHAS leo.
Dk. Elias Kwesi Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Daharura na Maafa Wizara ya Afya akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika MUHAS jana.
Baadhi ya wahitimu wa kozi hizo wakifuatilia hotuba za viongozi mbalimbali.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Zainab Chaula akimpongeza Mkuu wa Profesa Andrea Pembe Makamu Mkuu Chuo cha MUHAS mara baada ya kuzindua Muongozo wa kozi za Magonjwa ya Dharura na ajali.
Mkuu wa Profesa Andrea Pembe Makamu Mkuu Chuo cha MUHAS akizungumza mara baada ya kuzindua Muongozo wa kozi za Magonjwa ya Dharura na ajali.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Zainab Chaula akizungumza katika Chuo cha MUHAS mara baada ya kuzindua Muongozo wa kozi za Magonjwa ya Dharura na ajali.
Baadhi ya wadau kutoka vyombo mbalimbali kama TANROADS, Jeshi la Zimamoto, Polisi, JWTZ na Red Cross walioshiriki kutoa mafunzo kwa wahitimu wa mafunzo hayo.
Baadhi ya wahitimu mbalimbali wakikabidhiwa vyeti vyao na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Zainab Chaula.
Dk. Edwiga Swai kutoka Hospitali ya Muhimbili akitoa shukurani zake kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Zainab Chaula.