Mwanasheria kutoka Ofisi ya Msajili wa NGO Bi.Happy Msimbe akitoa huduma kwa Mmoja wa mdau kutoka Taasisi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ambayo awali yalisajiliwa chini ya Sheria nyingine akipata huduma ya kusajili Taasisi yake chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019 katika zoezi linaloendelea kufanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa kanda ya Mashariki.
Mwanasheria kutoka Ofisi ya Msajili wa NGO Bi. Idda Kombe akitoa huduma kwa Mmoja wa mdau kutoka Taasisi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ambayo awali yalisajiliwa chini ya Sheria nyingine akipata huduma ya kusajili Taasisi yake chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019 katika zoezi linaloendelea kufanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa kanda ya Mashariki.
Wanasheria kutoka Ofisi ya Msajili wa NGO kutoka kulia ni Denis Bashaka, wa pili kulia ni January kitunsi na wa pili kushoto Faki Shaweji wakifafanua jambo kwa Mmoja wa mdau kutoka Taasisi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ambayo awali yalisajiliwa chini ya Sheria nyingine akipata huduma ya kusajili Taasisi yake chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019 katika zoezi linaloendelea kufanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa kanda ya Mashariki.
Msajili na Mkurugenzi wa Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Vickness Mayao (Kushoto) akimsikiliza kwa makini aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi. Neema Mwanga wakati wa zoezi la kusajili Taasisi na Mashirika yaliyosajiliwa chini ya sheria nyingine kuja chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019 katika zoezi linaloendelea kufanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa kanda ya Mashariki.
***************
Na Mwandishi Wetu
Wadau kutoka Taasisi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini ambao awali walisajiliwa katika Sheria nje ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wameridhishwa na kasi ya uhuishaji wa usajili wa Taasisi na Mashirika hayo.
Hayo yamebainika leo jijini Dar es Salaam wakati wa zoezi linaloendelea la kuhuisha usajili wa Taasisi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ambayo awali yalisajiliwa chini ya Sheria nyingine ikiwemo “Societies Act Cap 337” (Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi) ; “Trustees’ Incorporation Act Cap. 318 (RITA); na The Companies Act Cap 212 (Msajili wa Makampuni-BRELA) ambazo zinatakiwa kujisajili chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019.
Wakizungumza wakati wa zoezi hilo mmoja wa wadau kutoka Shirika la ‘SOS Village Children’ Bw. Dhiyant Patel Patel amesema kuwa Shirika lao lilikuwa limesajiliwa chini ya Sheria ya “Trustees’ Incorporation Act Cap. 318 (RITA) hivyo kuhitajika kujisajili chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019.
Bw. Patel ameongeza kuwa zoezi hilo lina umuhimu na manufaa kwa Taasisi na Mashirika hayo kwani litawasaidia kuendelea kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa mujibu wa Sheria na taratibu zilizopo.
“Niwapongeze Wizara na kwa hatua hii ya kasi ya kuhuisha usajili wa Mashirika yaliyokuwa nje ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini sisi tumeitikia wito na tuko pamoja katika hili” alisisitiza Bw.Patel
Bw.Patel ametoa wito kwa Mashirika yanayotakiwa kujisajili chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019 kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo ili kuondokana na usumbufu mara baada ya Serikali kukamilisha zoezi hilo.
“Zoezi hili linaenda vizuri na hatukuamini kwamba tunaweza tukapata huduma hii kwa muda wa masaa mawili kusajili na kupata cheti husika” alisema.
Naye Mwakilishi wa Shirika la Bunjiri Community Development Support Bw. Ernest Mwanzi amesema kuwa Serikali imefanya jambo la muhimu kwa kuendesha zoezi hili kikanda na kushauri zoezi ili liendelee kufanyika katika mikoa mbalimbali nchini.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Haki Ardhi Bi. Gloria Msaki ameipongeza Wizara na Ofisi ya Msajili wa NGO kwa kujipanga katika zoezi la uhuishaji wa Taasisi na Mashirika yaliyosajiliwa katika Sheria nyingine ambayo yanatakiwa kujisajili chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019.
Akizungumza katika zoezi hilo Msajili na Mkurugenzi wa Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Vickness Mayao amesema kuwa utaratibu wa usajili umerahisishwa sana hasa ule wa Mashirika yalikuwa yamesajiliwa katika Sheria nyingine.
Ameongeza kuwa Wadau wameridhishwa na huduma zinazotolewa na Ofisi yake na kusema wanapata mrejesho mzuri kutoka kwa wadau kupitia fomu za mrejesho wa zoezi hilo.
Ofisi ya Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali inaendelea na zoezi la usajili wa Mashirika yaliyosajiliwa awali chini ya Sheria nyingine kama vile “Societies Act Cap 337” (Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nch); “Trustees’ Incorporation Act Cap. 318 (RITA); na The Companies Act Cap 212 (Msajili wa Makampuni-BRELA) ambazo zinatakiwa kujisajili chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019.
Usajili huu umeanza katika Kanda ya Mashariki (Dar es salaam, Lindi, Mtwara, Pwani na Morogoro) na Kituo kitakuwa Ofisi za Wizara ya Afya-Dar es Salaam kuanzia tarehe 10-19/07/ 2019.