Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amesema Bahi ni miongoni mwa Halmashauri bora Nchini katika suala zima la ujenzi unaoendelea wa Hospital za Wilaya.
Mhe. Jafo ametoa kauli hiyo wakati alipotembelea Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospital ya Wilaya.
Mhe. Jafo alifurahi kuona ujenzi wa hospitali ya Bahi ukiwa katika hatua za ukamilishaji na majengo yote yakiwa katika ubora wa hali ya juu.
“Ninyi ni miongoni mwa Halmashauri bora katika ujenzi wa hospitali ya Wilaya mmefanya kazi kubwa na nzuri ya usimamizi makini mbali na changamoto mlizokutana nazo hakika mmenifurahisha hongereni sana kwa kazi nzuri” Alisema Jafo.
Majengo yenu yote saba yako katika hatua ya ukamilishaji nimeshuhudia jitahada zenu za dhati, sababu nyie mlichelewa kuanza ujenzi na mmewahi kumaliza lakini kuna halmashauri zingine hawakuwa na changamoto yeyote na hawajafikia hatua ambayo mmefika Bahi aliongeza Jafo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe. Mwanahamis Munkunda ameelezea namna amnavyo walifanikiwa katika ujenzi huo kuwa waligawa majengo yote kwa Wakuu wa Idara kwa ajili ya usimamizi na ufuatiliaji na hawakumuachia mhandisi na mganga mkuu pekee katika kazi ya ujenzi wa hospitali.
“Umoja wetu ndio mafanikio yetu hii ndio imetusaidia kufanikisha kazi hii kwa wakati tumeshirikiana katika kusimamia na kufuatilia na kila jengo hapa unaloliona lina Mkuu wake wa Idara ambaye yeye ndiye anajua kila kinachohitajika au kilichopungua hii imetusaidia kufanya kazi ya ujenzi kwenda haraka alisema Munkunda.
Mhe. Jafo anaendelea na ziara yake katika Halmashauri zingine kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospital za Wilaya.