Picha ya pamoja ikionyesha baadhi ya washiriki katika kongamano la mashindano ya vyama vya umwagiliaji lililofanyikaJijini Dodoma Leo.
Bi Frida Tarimo Mkulima wa zao la Mpunga kutoka katika skimu ya kiloimocha Umwagiliaji Simanjiro akiongea kuhusu manufaa wanayopata kutokana na mafunzo ya utunzaji na uendeshaji wa miundombinu ya umwagiliaji, katika kongamano la mashindano ya vyama vya wamwagiliaji lililofanyika jijini Dodoma.
katika picha ni sehemu ya washiriki katika kongamano la mashindano ya vyama wa Umwagiliaji lilifanyika Jijini Dodooma leo.
Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo na Utafiti kutoka Wizara ya Kilimo Bw. Wilhelm Mafuru, akifungua kongamano la mashindano ya vyama vya umwagiliaji kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Mathew Mtigumwe leo Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu mstaafu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mbogo Mfutakamba akiongea na waandishi wa habari hawapo katika picha kuhusu umuhimu wa kilimo cha umwagiliaji na Tanzania ya viwanda.
……………………….
Na; Mwandishi Maalum – Dodoma
Wakulima wa Kilimo cha Umwagiliaji nchini kupitia Skimu za umwagiliaji, wametakiwa kuwa na usimamizi thabiti wa skimu hizo ili kilimo hicho kuwa cha uhakika zaidi na chenye tija kwa mkulima na taifa kwa ujumla.
Akimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya KIlimo Mhandisi Mathew Mtigumwe, Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo na Utafiti Bw. Wilhelm Mafuru, ameyasema hay o leo Jijini Dodoma katika kongamano kubwa lililoshirikisha vyama 36 na kushindanisha vyama vya umwagliaji 8 kutoka Kanda 8 za Umwagiliaji lenye lengo la kutoa motisha kwa skimu zilizowahi kupata mafunzo ya Matunzo na Uendeshaji chini ya Mradi wa kujenga uwezo kwa wataalamu wa Umwagiliaji wa TANCAID awamu wa pili kupitia Shirika la kimataifa la maendeleo la Japan JICA kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji. Kadhalika warsha imetoa fursa kwa wadau wa umwagiliaji kuona namna ya kuendeleza miundombinu ya umwagiliaji, pamoja na kutoa nafasi kwa vyama vya umwagiliaji kubadilishana uzoefu wa namna bora ya kuendesha na kutunza skimu za umwagiliaji.
Bw. Mafuru Amesema kuwa, tume ya Taifa ya Umwagiliaji imeendelea kusaidia wakulima kupata elimu kupitia wataalam ili kuweza kulima kwa tija na kuendelea kusimamia kuimarisha shughuli za kilimo cha umwagiliaji.
Akiongea kwa Niaba ya wakulima wa Skimu ya umwagiliaji ya Lemkuna Bi. Frida Tarimo, alisema kupitia mafunzo wanayopata wakulima wameweza kusimamia Uendeshaji na Matunzo ya miundombinu ya umwagiliaji, upatikanaji wa maji ya kutosha kwa vitalu na maandalizi mazuri ya kalenda ya msimu wa kilimo jambo ambalo ameeleza limeongeza uzalishaji katika kilimo hususan cha zao la Mpunga.
Awali akiongea na waandishi wa Habari Katibu Mkuu mstaafu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mbogo Futakamba alisema kuwa kuelekea Tanzania ya Viwanda kilimo cha umwagiliji kinahitaji uwekezaji mkubwa na miundombinu bora na mfumo sahihi wa umwagiliaji jambo ambalo linaweza kuleta uhakika wa chakula malighafi za viwanda na kilimo kuboreka kupitia mifumo sahihi ya umwagiliaji.