Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakati wa ufunguzi wa uhuishaji zoezi la usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ambayo awali hayakusajili chini ya Sheria Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii akieleza lengo la Mkutano wa Wizara na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakati wa ufunguzi wa uhuishaji zoezi la usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yale ambayo awali hayakusajili chini ya Sheria Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akijadiliana jambo na mmoja wa wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mara baada ya ufunguzi wa uhuishaji zoezi la usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ambayo awali hayakusajili chini ya Sheria Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
Wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakifuatilia jambo wakati wa ufunguzi wa uhuishaji zoezi la usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yale amabayo awali hayakusajili chini ya Sheria Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
……………………
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Na Anthony Ishengoma- WAMJW
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amemwagiza Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi. Vickness Mayao kuandaa mazingira rafiki yakuwezesha zoezi la uhuishaji usajili wa Mashirika Yasiyo ya kiserikali kwa kutayarisha mfumo wa kieletroniki kufanyika kwa wiki mbili utakaowezesha uhuishaji huo.
Naibu Waziri Ndugulile ametoa agizo hilo leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua zoezi la uhuishaji usajili mpya wa NGOs ambazo awali zilifanya usajili wake kwa Sheria nyingine ikiwemo ya makampuni chini ya Brela na kutakiwa kusajili upya baada ya Sheria ya Msajili wa NGOs kufanyiwa Marekebisho na Bunge.
Naibu Waziri Ndugulile katika maagizo yake kwa Msajili huyo amemtaka kuhakikisha anatumia mfumo wa Kieletroniki ili mashirika yailiyombali na maeneo ya vijijini waweze kutumia mtandao huo kupata taarifa za muhimu na kukamilisha zoezi hilo bila kusafili mbali kufuata huduma ya usajili akiongeza kuwa zoezi hilo litamwezesha msajili kufanya kazi hiyo katika muda uliopangwa.
“Nataka wadau wote wafanye kazi vizuri natoa wiki mbili zoezi hili liwemekamilika, wekeni mfumo mzuri wa kielektroniki ili wadau wote wafanye kazi katika mazingira mazuri kwani itakuwa ni aibu kubwa kwa mtu kusafiri kutoka Tanga kufuata karatasi Dodoma’’ Aliongeza Dkt. Ndugulile.
Dkt. Ndugulile amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha Mashirika husika yanayofanya kazi ya aina moja na kusajili chini ya Sheria husika kwa lengo la kuweka vizuri usimamizi wa Mashirika hayo na kuwatoa wasiwasi Mashirika Yasiyo ya Kiserikali hususani Mashirika ya Kimataifa kwa kuyataka kufahamu vema malengo mazuri ya Serikali ya kuwahakikisha usimamizi mzuri Mashirika yote yanayofanya kazi zisizo za faida.
Dkt. Ndugulile amewahakikisha kuwa Serikali yake ina dhamira nzuri kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwani Serikali itatoa cheti cha muda maalum wa miaka kumi tofauti na nchi nyingine ambazo cheti utolewa kwa mwaka mmoja na kuonya kuwa kama Serikali yake ingekuwa na dhamira mbaya ingetoa cheti hicho kila mwaka kama zilivyo nchi jirani hivyo kuwataka wadau wa Mashirika haya kutokuwa na wasiwasi.
Wakati huohuo Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema lengo ni kujadiliana kwa pamoja hili kujenga uelewa wa pamoja kuhusu sheria mpya Na. 3 ya mwaka 2019 na kupokea maoni ya wadau kuhusu usajili na uhuishaji wa mashirika haya.
Aidha Dkt. Jingu aliongeza kuwa kutokana marekebisho ya Sheria hii Wizara na Wadau wanakaa pamoja kujenga maelewano na kupeana elimu ili wote kwa pamoja waweze kuhitimisha wasiwasi na uoga uliokuwepo kutokana na mabadiliko mapya ya Sheria.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Foundation for Civil Society Bw. Francis Kiwanga amesema kuwa mabadiliko ya Sheria kimsingi ni fursa ya kuratibu vizuri zaidi Mashiriki lakini pia kuweka na kutambua Mchango wa Mashirika kwa maendeleo ya Taifa kwani ilikuwa ni vigumu kufanya hivyo wakati mashirika haya yalpokuwa kwa wasimamizi tofauti tofauti.
Naye Mkurugenzi wa Shirika la REPSSI Bi. Edwick Mapalala ameongeza kuwa wasiwasi uliokuwepo kwa Mashirika umekwisha kufuatia ufafanuzi wa Naibu Waziri Ndugulile na kuyahimiza Mashirika kushirikiana na Wizara kwani Taasisi yake ni kielelezo baada ya kufanikiwa kufanya kazi na Serikali ya Mkoa wa Kagera kwani ni moja ya Taasisi chache zinafanya kazi Wilayani Kyelwa tofauti na Taasisi nyingi kurundikana katika Wilaya moja.
Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii leo imeanza rasmi uhuishaji wa usajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali yale ambaye awali yalijisajili chini ya sheria nyingine ikiwemo sheria ya makampuni iliyo chini ya Brela na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi lakini Mashirika hayo kazi zake ni zile zisizo za kifaida ambazo zinajisajili upya kwa mujibu wa sheria ya Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.