NJOMBE
Halmashauri ya mji wa Njombe imevifikisha mahakamani vikundi 47 vya wajasiriamali ambavyo vimeshindwa kurejesha fedha za mikopo ya asilimia kumi zitokanazo na mapato ya ndani ikiwa na lengo la kuhimiza urejeshwaji ili wahitaji wengine waweze kukopeshwa.
Zaidi ya mil 98 zimeshindwa kurejeshwa tangu mwaka 2015 hadi sasa jambo ambalo limeibua hoja kwa mkaguzi wa hesababu za serikali CAG ambaye ameshauri halmashauri kuhakikisha zinatoa mikopo hiyo kwa wajasiriamali na kuzifatilia kwa marejesho ili ziweze kutumika kukopesha wahitaji wengine
Dorcas Mkello ambaye ni mhazina wa halmashauri ya mji wa Njombe akiwasirisha hoja kwa niaba ya mkurugenzi amesema halmashauri imekuwa na changamoto kubwa katika kufatilia wadaiwa wa mikopo ya asilimia kumi na kudai kwamba kitendo hicho kumekwamisha mipango ya halmashauri ya kuwawezesha mitaji wajasiriamali
Mbali na suala hilo imejadiliwa pia changamoto kubwa ya miundombinu ya shule pamoja na upungufu wa vyumba vya madarasa ambalo lilisababisha baadhi ya wanafunzi waliofaulu kidato cha kwanza kwenda shule binafsi kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa ambapo baadhi ya madiwani akiwemo Ditrick Msemwa, George Sanga na Agrey Mtambo wanasema endapo kungekuwepo na mshikamano baina ya pande zote lingekuwa limetatuliwa huku matamko na kauli za viongzi zikitajwa kuwa kikwazo.
Zoezi la ujenzi wa madarasa na shule mpya ambalo linaendelea kwa baadhi ya kata za halmashauri ya mji wa Njombe limetajwa kukwamishwa na zuio la kuwachangisha wananchi kufanikisha ujenzi huo jambo ambalo linapokelewa tofauti na mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka ambae anatoa ruhusa kwa watendaji na madiwani kwa kibali chake kuwachangisha wananchi ili kukamilisha ujenzi madarasa kabla ya 2020.
licha ya halmashauri ya mji wa Njombe kuwa na changamoto nyingi katika utekelezaji wa miradi yake lakini halmashauri ya mji wa Njombe ni miongoni mwa halamshauri ya tano kati ya sita ambazo zimepata hati safi isipokuwa Makete.