……………………
Na Mwandishi Wetu
KATIKA kuhakikisha azma ya serikali ya awamu ya tano ya kuwa na uchumi wa kati unaotegemea viwanda ifikapo Mwaka 2025 inatimia, Benki ya Biashara ya DCB imeingia na mpango kabambe wa kuviwezesha viwanda vya kilimo kwa kuja na bidhaa maalum ya DCB SOKONI ambayo inatoa suluhisho la kudumu kwa wakulima na wenye viwanda huku ikilenga kuwawezesha wakulima na wafanyabiashara kiuchumi.
Bidhaa hii mpya itamuwezesha mfanyabiashara mwenye azma ya kufungua viwanda vya kilimo kupata mikopo ya kuanzisha viwanda vya kilimo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa bidhaa hiyo ukiofanyika pamoja na uzinduzi wa kiwanda kipya cha kukoboa mpunga cha mteja wao Bwana Callington kayuni, kilichopo katika kijiji cha Mlowo Mbozi Mkoa wa Songwe juzi, Mkurugenzi wa Biashara wa benki hiyo, James Ngaluko alisema ‘tunayo furaha kubwa leo kushiriki kwenye uzinduzi huu muhimu na wa tija wa kiwanda hichi kikubwa na cha kisasa cha kukobolea mpunga kilichojengwa kwa uwezeshwaji mkubwa wa Benki ya biashara ya DCB, tunaamini kiwanda hichi kitakuwa mkombozi wa kweli kwa wakulima wanaofanya shughuli zao za kilimo katika kijiji hichi na vijiji vilivyopo karibu na hapa.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa kwa kuleta bidhaa hii mahususi ya DCB Sokoni, itawawezesha wafanyabiasha na wakulima sasa kufanya mapinduzi ya kweli kiuchumi kwa kutegemea kilimo pamoja na minyororo ya thamani kwani kupitia DCB tunakuongezea thamani ya mazao ya mkulima.
Alizitaja njia ambayo bidhaa ya DCB Sokoni itamuwezesha mteja kuwa ni pamoja na Kujenga kiwanda, kununua na kusafirisha mazao kutoka shambani, kuuza mazao ghafi au Kuchakata mazao na kuyaongezea thamani, usambazaji kwenda sokoni kwa wateja, ulinzi kutokana na bima ya maisha, kiwanda, pamoja na mazao ghalani katika kipindi chote cha mkopo, ununuaji wa nyumba ya makazi (Mortgage loan) utakaomwezesha kulipa taratibu kwa kipindi kirefu, ununuaji wa pembejeo kwa wafanyabiashara wa pembejeo na zana za kilimo, ubadilishaji wa fedha za kigeni zitokanazo na mauzo ya mazao na uwekezaji wa fedha kwa faida nzuri kupitia huduma ya DCB Lamba Kwanza.
“Natoa wito kwa wateja na wasio wateja kujiunga na DCB sokoni kwani tunatoa mikopo ya bei nafuu sana ambapo mkulima, mfanya biashara hawezi kushindwa kulipa na pia tunatoa thamani kwa mazao yako ili mteja aweze kushindana kwenye soko na bidhaa zake zinufaike na mnyororo wa thamani”, aliongeza Bwana Ngaluko.
Pamoja na hayo alisema uwezeshwaji wa viwanda vya kilimo kama ilivyo katika kiwanda hichi cha mteja wetu cha kukoboa mpunga, utachangia kwa kiasi kikubwa kasi ya uwekezaji kwa watanzania. Vilevile uwezeshaji huu utasaidia pia kuongeza kiasi cha mazao ya biashara yanayouzwa nje ya nchi, mazao ya biashara kama pamba, kahawa, korosho na mengineyo, hivyo kutuletea fedha za kigeni na kuinua pato la Taifa.
“Ni matumaini yetu wakulima na wafanyabiashara wa mkoa wa Songwe na maeneo jirani wataleta mazao yao katika kiwanda hiki hivyo kuweza kupata chakula na biashara itakayowaongezea kipato na kuinua maisha yao.
“Benki inaunga mkono juhudi za serikali katika kuiwezesha sekta ya kilimo kifedha, sekta hii inakabiliwa na changamoto nyingi, baadhi ikiwa ni ukulima unaotegemea mvua za msimu na changamoto za upatikanaji wa masoko, kupitia DCB Sokoni ni imani yetu tutaweza kuleta ufumbuzi wa baadhi ya changamoto hizo,” alisema mkurugenzi huyo.
Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi na Mmiliki wa kiwanda hicho, Callington Kayuni aliishukuru Benki ya DCB kwa uwezeshaji wa kifedha alioupata uliowezesha ujenzi wa kiwanda hicho kutoka hatua ya awali mpaka mwisho kiwanda chenye uwezo wa kukoboa hadi magunia 350 kwa siku.
“Nilipeleka michanganuo ya kuomba msaada wa kifedha katika Taasisi nyingi za Fedha, naishukuru DCB kwasababu walilipokea andiko langu kwa mikono miwili na matokeo yake ndio haya ambayo kila mmoja wenu anashuhudia kwa macho yake uwekezaji huu tulioufanya hapa Karacha, wilayani Mbozi,” alisema.
Hata hivyo Mkurugenzi huyo alitaja changamoto ya masoko kuwa ni moja ya mambo yayozorotesha ufanisi wa kiwanda kwani wakulima wanaoleta mpunga kukobolewa kiwandani hapo hutegemea kupata soko hapo hapo la mchele hivyo wapo mbioni kuomba mkopo wa kifedha kutoka DCB utakaowezesha suala hilo.
Naye Richard Mwailanga aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mbozi katika hafla hiyo alisema serikali katika wilaya ya Mbozi inaunga mkono juhudi za Taasisi za Fedha Kama DCB katika uwezeshaji wa viwanda kwani viwanda hivyo vinasaidia kuongeza mapato na pia kukuza uchumi kwa wakazi wa eneo hilo.
Pamoja na hayo aliongeza uanzishwaji wa viwanda kama hivyo utapunguza changamoto iliyopo sasa ya wakulima kuuza mazao yao yakiwa hayajatayarishwa jambo linalofanywa mazao yao kuuzwa kwa bei ya chini.
“Wakulima wengi wa Mbozi wangependa pia kuchukua mikopo kama alivyofanya Bwana Kayuni baadhi wanaogopa kutokana na hofu ya urejeshaji wa mikopo na riba, natoa wito kwa taasisi za fedha kuweka utaratibu rafiki katika eneo hilo hususani katika mikopo inayowahusu wakulima na kilimo,”. Aliongeza
……………………Na Mwandishi WetuKATIKA kuhakikisha azma ya serikali ya awamu ya tano ya kuwa na uchumi wa kati unaotegemea viwanda ifikapo Mwaka 2025 inatimia, Benki ya Biashara ya DCB imeingia na mpango kabambe wa kuviwezesha viwanda vya kilimo kwa kuja na bidhaa maalum ya DCB SOKONI ambayo inatoa suluhisho la kudumu kwa wakulima na wenye viwanda huku ikilenga kuwawezesha wakulima na wafanyabiashara kiuchumi.Bidhaa hii mpya itamuwezesha mfanyabiashara mwenye azma ya kufungua viwanda vya kilimo kupata mikopo ya kuanzisha viwanda vya kilimo.Akizungumza wakati wa uzinduzi wa bidhaa hiyo ukiofanyika pamoja na uzinduzi wa kiwanda kipya cha kukoboa mpunga cha mteja wao Bwana Callington kayuni, kilichopo katika kijiji cha Mlowo Mbozi Mkoa wa Songwe juzi, Mkurugenzi wa Biashara wa benki hiyo, James Ngaluko alisema ‘tunayo furaha kubwa leo kushiriki kwenye uzinduzi huu muhimu na wa tija wa kiwanda hichi kikubwa na cha kisasa cha kukobolea mpunga kilichojengwa kwa uwezeshwaji mkubwa wa Benki ya biashara ya DCB, tunaamini kiwanda hichi kitakuwa mkombozi wa kweli kwa wakulima wanaofanya shughuli zao za kilimo katika kijiji hichi na vijiji vilivyopo karibu na hapa.Mkurugenzi huyo alisema kuwa kwa kuleta bidhaa hii mahususi ya DCB Sokoni, itawawezesha wafanyabiasha na wakulima sasa kufanya mapinduzi ya kweli kiuchumi kwa kutegemea kilimo pamoja na minyororo ya thamani kwani kupitia DCB tunakuongezea thamani ya mazao ya mkulima.Alizitaja njia ambayo bidhaa ya DCB Sokoni itamuwezesha mteja kuwa ni pamoja na Kujenga kiwanda, kununua na kusafirisha mazao kutoka shambani, kuuza mazao ghafi au Kuchakata mazao na kuyaongezea thamani, usambazaji kwenda sokoni kwa wateja, ulinzi kutokana na bima ya maisha, kiwanda, pamoja na mazao ghalani katika kipindi chote cha mkopo, ununuaji wa nyumba ya makazi (Mortgage loan) utakaomwezesha kulipa taratibu kwa kipindi kirefu, ununuaji wa pembejeo kwa wafanyabiashara wa pembejeo na zana za kilimo, ubadilishaji wa fedha za kigeni zitokanazo na mauzo ya mazao na uwekezaji wa fedha kwa faida nzuri kupitia huduma ya DCB Lamba Kwanza.“Natoa wito kwa wateja na wasio wateja kujiunga na DCB sokoni kwani tunatoa mikopo ya bei nafuu sana ambapo mkulima, mfanya biashara hawezi kushindwa kulipa na pia tunatoa thamani kwa mazao yako ili mteja aweze kushindana kwenye soko na bidhaa zake zinufaike na mnyororo wa thamani”, aliongeza Bwana Ngaluko.Pamoja na hayo alisema uwezeshwaji wa viwanda vya kilimo kama ilivyo katika kiwanda hichi cha mteja wetu cha kukoboa mpunga, utachangia kwa kiasi kikubwa kasi ya uwekezaji kwa watanzania. Vilevile uwezeshaji huu utasaidia pia kuongeza kiasi cha mazao ya biashara yanayouzwa nje ya nchi, mazao ya biashara kama pamba, kahawa, korosho na mengineyo, hivyo kutuletea fedha za kigeni na kuinua pato la Taifa.“Ni matumaini yetu wakulima na wafanyabiashara wa mkoa wa Songwe na maeneo jirani wataleta mazao yao katika kiwanda hiki hivyo kuweza kupata chakula na biashara itakayowaongezea kipato na kuinua maisha yao.“Benki inaunga mkono juhudi za serikali katika kuiwezesha sekta ya kilimo kifedha, sekta hii inakabiliwa na changamoto nyingi, baadhi ikiwa ni ukulima unaotegemea mvua za msimu na changamoto za upatikanaji wa masoko, kupitia DCB Sokoni ni imani yetu tutaweza kuleta ufumbuzi wa baadhi ya changamoto hizo,” alisema mkurugenzi huyo.Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi na Mmiliki wa kiwanda hicho, Callington Kayuni aliishukuru Benki ya DCB kwa uwezeshaji wa kifedha alioupata uliowezesha ujenzi wa kiwanda hicho kutoka hatua ya awali mpaka mwisho kiwanda chenye uwezo wa kukoboa hadi magunia 350 kwa siku.“Nilipeleka michanganuo ya kuomba msaada wa kifedha katika Taasisi nyingi za Fedha, naishukuru DCB kwasababu walilipokea andiko langu kwa mikono miwili na matokeo yake ndio haya ambayo kila mmoja wenu anashuhudia kwa macho yake uwekezaji huu tulioufanya hapa Karacha, wilayani Mbozi,” alisema.Hata hivyo Mkurugenzi huyo alitaja changamoto ya masoko kuwa ni moja ya mambo yayozorotesha ufanisi wa kiwanda kwani wakulima wanaoleta mpunga kukobolewa kiwandani hapo hutegemea kupata soko hapo hapo la mchele hivyo wapo mbioni kuomba mkopo wa kifedha kutoka DCB utakaowezesha suala hilo.Naye Richard Mwailanga aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mbozi katika hafla hiyo alisema serikali katika wilaya ya Mbozi inaunga mkono juhudi za Taasisi za Fedha Kama DCB katika uwezeshaji wa viwanda kwani viwanda hivyo vinasaidia kuongeza mapato na pia kukuza uchumi kwa wakazi wa eneo hilo.Pamoja na hayo aliongeza uanzishwaji wa viwanda kama hivyo utapunguza changamoto iliyopo sasa ya wakulima kuuza mazao yao yakiwa hayajatayarishwa jambo linalofanywa mazao yao kuuzwa kwa bei ya chini.“Wakulima wengi wa Mbozi wangependa pia kuchukua mikopo kama alivyofanya Bwana Kayuni baadhi wanaogopa kutokana na hofu ya urejeshaji wa mikopo na riba, natoa wito kwa taasisi za fedha kuweka utaratibu rafiki katika eneo hilo hususani katika mikopo inayowahusu wakulima na kilimo,”. Aliongeza