Home Teknolojia AUTO-ELECTRIC PANEL KIFAA CHA KUFUNDISHIA KWA VITENDO KATIKA UMEME WA VIWANDANI NA...

AUTO-ELECTRIC PANEL KIFAA CHA KUFUNDISHIA KWA VITENDO KATIKA UMEME WA VIWANDANI NA MIGODINI

0

mwanagenzi kutoka VETA-Moshi, Bw. Sadick Ngonyani akionesha mfano wa mtambo wa umeme unaotumika katika Migodi, Magari makubwa pamoja na Viwandani katika maonesho ya biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

NA EMMANUEL MBATILO

Chuo cha Ufundi Stadi  VETA-Moshi kupitia mafunzo ya uwanagenzi (Apprenticeship) mbayo yanatolewa na Tanzania Chamber of Miniral (TCM) kwa kushirikisha makampuni ya uchimbaji wa madini kama vile Acacia na matawi yake,Geita gold Mining,Shant gold Mining pamoja na makampuni mbalimbali hapa nchini wameandaa program hiitwayo Auto-Electric Panel ambayo inaruhusu mwanagenzi kupata muda wa kujifunza kwa vitendo kablya kuingia katika chombo..

Ameyasema hayo leo mwanagenzi kutoka VETA-Moshi, Bw. Sadick Ngonyani katika maonesho ya biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Fullshangwe blog amesema kuwa program hiyo inamuwezesha mwanagenzi kupata uelewa wa haraka katika mitambo na mashine mbalimbali za migodi, viwandani na hata katika magari yanayotumia diesel.

 Kwa upande wake mratibu wa mafunzo ya uwanagenzi VETA_Moshi, Bi.Theresia Ibrahimu amesema kuwa mfumo huo wa  ufundishaji kwa vitendo na natharia kwa kutumia mitambo ya kisasa kama vile umeme wa magari makubwa na mitambo kabla ya mwanagenzi kwenda kwenye chombo halisi.

Bi. Theresia amemaliza kwa kusema kuwa mfumo wa Uwanagenzi VETA-Moshi unatolewa katika fani mbalimbali nje ya fani ya Auto-Electricikiwemo Plater Wedding,Filting and Machining, Heavy duty Machine pamoja na Industrial Electrical Fitter.