Picha mbalimbali zikionesha wananchi wakipata maelezo wakati walipotembelea banda la Watumishi Housing Company shirika ambalo imeibuka Mshindi wa pili katika kundi la Washiriki wa Kundi la Wajenzi na Wauzaji Nyumba kwenye maonesho ya 43 ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya JK Nyerere Jijini Dar es salaam.
……………………………………………
Ofisa Uhusiano na Masoko MaryJane Makawia amesema,Mfuko wa pamoja wa uwekezaji katika milki wa Watumishi Housing Company umeibuka kuwa washindi wa pili wa tuzo ya mabanda ya ujenzi na wauzaji nyumba Bora iliyokabidhiwa na Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu.
MaryJane Makawia amesema wamefurahia tuzo hiyo na imewapa ari mpya ya kujipanga ili mwakani waweze kuibuka mshindi wa Kwanza katika maonesho mengine ya mwakani.
Tuzo hizo zilitolewa Julai 1 jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa Maonyesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
“Tuzo hii ni thamani kubwa kwetu imetupa moyo kwamba kazi yetu inakubalika na inaonekana kwa jamii hivyo tutajipanga mwakani tutakuwa wa Kwanza,”alisema MaryJane.
Akizungumzia Ushirikiano wao kwenye Maonyesho ya mwaka huu alisema wamekuja na bidhaa mbili ambazo zimelenga kunufaisha jamii nzima.
Alisema katika mabanda yao wamekuja na huduma za kupangisha nyumba zao kwa gharama nafuu kusnzia Sh.150 Hadi 350,000 ambazo zipo Bunju, Kigamboni, Mwanza na Morogoro.
MaryJane alisema pia wameanza kuongeza wigo kwa wateja wa sekta binafsi na wanachama wa mifuko ya jamii.
“Kwa Sasa njia za malipo zimeongezeka ambapp mteja mwenyewe anaweza kununua kwa mikopo ya muda mfupi,”alisema MaryJane.
Alisema kwa wateja watakaofika 77 huduma zote zinapatikana ikiwamo kuonyeshwa picha ya mradi, Bei wake na ujazwaji fomu.
Hata hivyo alisema wanakabiliwa na changamoto ya wataanzania kukosa elimu sahihi ya umuhimu wa kununua nyumba za mfuko huo.
Alisema imekuwa kawaida wataanzania kujenga Imani potofu kuwa nyumba ni lazima wajenge wao wenyewe Hali inayosababisha wengi wao kushindwa kumiliki nyumba hadi Sasa na kutumia fedha nyingi kupanga.