Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa
Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola, akikagua ujenzi wa darasa wa
Shule ya Msingi Kamulebya, Kijiji cha Buzimbwe, Kata ya
Butimba, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara,
wakati Mbunge huyo alipofanya ziara katika kijiji hicho kusikiliza
kero za wapigakura wake pamoja na kuwataka wananchi
wachape kazi. Waziri Lugola pia alitembelea miradi mbalimbali ya
maendeleo, ikiwemo ujenzi wa madarasa ya shule na Zanahati.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkazi wa Kijiji cha Kamulebya, Kata ya Butimba, Jimbo la
Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, Wambura Chacha Wambura, akimuuliza swali Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kulia), wakati Mbunge huyo alipofanya ziara katika kijiji hicho kusikiliza kero za wapigakura wake pamoja na kuwahamasisha
kufanya kazi. Lugola aliwapa nafasi wananchi kutoa kero zao
ndani ya Jimbo lake. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa
Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kushoto), akimsalimia Diwani wa
Kata ya Butimba, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa
Mara, Abyudi Mugesi, wakati alipokuwa anawasili Kijiji cha
Buzimbwe kwa ajili ya kufanya Mkutano wa hadhara na wananchi
wa Kijiji hicho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.