************
LICHA ya juhudi kubwa zinazofanywa na serikali pamojana na mashirika mbalimbali ya kutetea haki za binadamu na vitendo vya ukatili wa kijinsia, lakini inaelezwa kuwa bado mkoani Dodoma vitendo hivyo vinazidi kushamili katika maeneo mbalimbali mkoani humo.
Akizungumza na wanahabari juu ya utendaji wa jeshi la polisi mkoani humo, Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, Kamishna msaidizi wa polisi, Gilles Muroto amebainisha kuwa vitendo hivyo vimezidi kushamimiri mkoani humo, amesema katika tukio la kwanza.
Katika kijiji cha Mlazo, tarafa ya Mpyayungu, Wilaya ya Chamwino, Makame Wambura, (28) na mtoto wake Fidelika Walioba miezi mitatu(3) baada ya kumwagiwa mafuta ya petrol na mume wake aitwae Elias Warioba (30) na wote wawili kujeruhiwa vibaya na wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma, na hapa kamanda anaelezea tukio lilivyotokea.
“Mnamo tarehe28,06,2019, katika jiji cha Mlazo Tarafa ya Mpyayungu Wilayani chamwino, Makame Wambura(28) na motto wake miezi 3 walijeruhiwa kwa kuchomwa moto baada ya kumwagiwa mafuta ya petrol na mume wake Elias Warioba” amesema.
Tukio la pili katika kijiji cha Manchali, tarafa ya Chilonwa, Wilayani Chamwino, walimkamata Mazengo Chilatu(28) kwa kosa la kumlawiti mama yake mzazi ambaye hakujulikana jina wala umri wake kwa kumvizia akiwa amelala.
“Huko katika kijiji cha Manchali tarafa ya Chilonwa, wilaya ya Chamwino tumemkamata Mazengo Chilatu(28) kwa kosa la kumlawiti mama yake mzazi ambapo alimvamia alimvamia chumbani akiwa amelala na kumfanyia kitendo hicho” amesema.
Katika tukio la tatu huko katika eneo la Nane nane kata ya Nzuguni, Dodoma Mjini, kikongwe wa miaka 95, mkazi wa eneo hilo alibakwa na kijana mmoja Donald Justine(25) aliyemvizia akiwa amelala na kumkaba shingoni kasha kumtendea ubaya huo.
“Na katika eneo la nanenane kata ya nzuguni halmashauri ya Jiji la Dodoma kijana mmoja Donald Jastine (25) mkazi wa eneo hilo alimbaka bibi kizee mwenye umri wa miaka 95 kwa kumvamia na kumtendea kitendo hicho, chanzo ni ulevi uliopindukia na imani za kishirikina” amesema.
Lingine katika eneo la Maili mbili jijini humo ,ni tukio la Mwanaume mmoja anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 25- 30 ambaye hakufahamika jina lake alifanya matukio matatu ya ubakaji kabla ya kukamatwa na wananchi na kupigwa na wananchi kabla ya kuokolewa na polisi na baadaye kufariki.
Ambapo alifanya matukio hayo kwa watu watatu tofauti kabla ya jana kukamatwa na wananchi wenye hasira kali na kuupigwa vibaya na kuokolewa na jeshi la polisi hata hivyo alifariki baadaye.
Aidha amepongeza kazi nzuri inayofanyawa na wanahabari katika kuripoti habari za ukatili huo, ambapo amesema kwa sasa kumekuwa na mwamko mkubwa wa wananchi kuripoti matukio hayo kwa jeshi la polisi.
“kutokana na kuripoti kwenu habari hizi za ukatili tumeona sasa muamuko ni mkubwa sana kwa sasa katika kuripoti wananchi matukio haya yanapotokea katika maeneo yao” amesema.
Pia amebainisha kuwa matokeo ya kuripoti matukio hayo ambapo kwa mwaka 2018 yalilipotiwa matukio mia moja sabini a nne(174) na kwa mwaka 2019 ni matukio 517 ambapo kutokana na mwamko wa wananchi kuripoti kuna ongezeko la matukio 343.