Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kujadili kwa pamoja namna bora ya kuendeleza Kilimo Hifadhi nchini iliyofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakifatilia kwa karibu hotuba ya waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kujadili kwa pamoja namna bora ya kuendeleza Kilimo Hifadhi nchini iliyofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kilimo, Hifadhi Barani Afrika (ACT) Saidi Mkomwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kujadili kwa pamoja namna bora ya kuendeleza Kilimo Hifadhi nchini iliyofanyika leo jijini Dodoma
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Mhe Mahamoud Mgimwa ambaye ni Mbunge wa Mufindi Kaskazini akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kujadili kwa pamoja namna bora ya kuendeleza Kilimo Hifadhi nchini iliyofanyika leo jijini Dodoma
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akimkabidhi cheti cha pongezi Shaban Minja ambaye ni mkulima wa kilimo hifadhi kutoka Wilayani Same.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akimkabidhi cheti cha pongezi Bi Gloria Emmanuel ambaye ni mkulima wa kilimo hifadhi toka Wilaya ya Monduli.
Waziri wa Kilimo Mhe.Japhet Hasunga,akiwa katika picha ya pamoja na wadau baada ya kufungua warsha ya siku tatu ya kujadili kwa pamoja namna bora ya kuendeleza Kilimo Hifadhi nchini iliyofanyika jijini Dodoma.
………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
KATIKA kuhakikisha Tanzania inafikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 imeelezwa kuwa ni lazima iwekeze kikamilifu katika kilimo hifadhi ikiwa ni pamoja na kuhamasisha matumizi ya teknolojia za kisasa katika kilimo.
Hayo yamebainisha Jijini Dodoma na Waziri wa kilimo Japhet Hasunga, wakati akifungua Warsha ya Wadau wa Kilimo Hifadhi Tanzania.
Amesema serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki ikiwamo kumefuta kodi nyingi, amesema licha ya hayo lazima kuhamasishana matumizi ya Teknolojia za kisasa ambazo ni rafiki katika kilimo.
Amebainisha kuwa ni muhimu kujadiliana pamoja kuhusu sheria kwani hatuwezi kufika uchumi wa kati mwaka 2025 bila kufikia kilimo imara na chenye tija.
“Lazima kuimarishwe mafunzo kwani kilimo nchini bado kipo chini, pia tuongeze utafiti kwakuwa bila utafiti hakuna kilimo na lazima ijulikane kilimo gani kitumike,pembejeo gani zitumike,pia tuongeze uzalishaji wenye tija,” amesema Waziri Hasunga.
Katika kuimarisha na kuwapa uwezo wakulima amesema Serikali inakuja na mkakati wa bima kwa wakulima lengo likiwa ni kumsaidia mkulima pindi ambapo mazao yake yatakuwa yameharibika shambani.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Kilimo, Mifugo na Maji, Mahmoud Mgimwa amesema kama Serikali itawekeza katika kilimo hifadhi basi sekta ya kilimo itafika mbali.
Mgimwa ambaye ni Mbunge wa Mufindi Kaskazini (CCM) ameiomba Serikali kuongeza bajeti katika sekta ya kilimo hasa katika utafiti na kufanya mageuzi makubwa katika kilimo hasa katika sheria.
“Sera na sheria zina matatizo makubwa unakuta mkulima natayarisha shamba naanza kulima napalilia halafu wakati wa kuvuna Serikali inaanza kunipangia nikauze wapi sio sawa kabisa hapa ni lazima tutengeneze sheria nzuri” amesema Mgimwa.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kilimo, Hifadhi Barani Afrika(ACT) Saidi Mkomwa amesema kilimo hifadhi ni kilimo kinachozingatia uhifadhi wa rasilimali udongo na mazingira kwa ujumla.
Amesema kilimo hicho kimejengwa katika misingi mikuu mitatu ambayo ni kusumbua udongo,kuacha masalia shambani na kufanya kilimo mzunguko.
“Kilimo hiki ni cha miaka mingi na kilianza miaka 40 iliyopita Ulaya ila kwa Barani Afrika bado kipo nyuma ndio kimefika sasa ila ni kilimo chenye faida na tija kubwa kwa mkulima,”amesema Mkomwa.