Home Teknolojia VETA MKOANI SONGEA WAMETENGENEZA MASHINE MAALUMU KWAAJILI YA UBANGUAJI KOROSHO

VETA MKOANI SONGEA WAMETENGENEZA MASHINE MAALUMU KWAAJILI YA UBANGUAJI KOROSHO

0

Mwanafunzi wa Chuo cha Ufundi VETA Mkoa wa Songea,Bw. Kandidus Nchimbi akiwaonesha na kuwaelekeza wateja namna mashine ya kubangua korosho inavyofanya kazi katika maonyesho ya biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam

***********

NA EMMANUEL MBATILO

Chuo cha Ufundi VETA  Mkoa wa Songea kupitia kwa wanafunzi wake wametengeneza mashine ambayo itaweza kubangua korosho kwa ubora ili kuweza kumrahisisisha mtu kuondokana na ubanguaji holela kama ilivyozoeleka kwa baadhi ya watu.

Akizungumza na Fullshangwe blog katika maonyesho ya biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam, Mwanafunzi wa Chuo cha Ufundi VETA Mkoa wa Songea,Bw. Kandidus Nchimbi amesema kuwa wameamua kutengeneza mashine hiyo hiitwayo Cashewnutus Machine ambayo itasaidia ubanguaji korosho zisizochomwa wala kuchemshwa.

“Lengo la kutengeneza hiyo Mashine ni kumuwezesha mkulima ambaye anahusika na korosho asiwe na mchakato mingi kuiandaa korosho kumfikia mteja au mfanyabiashara”. Amesema Bw.Nchimbi.

Ameongeza kuwa wanahitaji kufikia malengo yao hasa kuwafikia wakulima wa korosho ambao wapo pembeni ili waweze kupata mashine hiyo kuweza kumrahisishia katika ubanguaji.

“Hii ni hatua ya kwanza katika utengenezaji wa mashine ya ubanguaji wa korosho, tunamashine ndogo ila tunampango wa kutengeneza mashine kubwa ambayo itakuwa rahisi kwa mkulima kuendena na kauri mbiu ya Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Tano John Magufuri kuwa Tanzania ya Viwanda”. Amesema Bw. Nchimbi.

Pamoja na hayo Bw. Nchimbi amewataka wakulima kutumia mashine katika ubanguaji korosho kuliko kutumia mawe na njia nyingine zisizokuwa salama kwa matumizi ya chakula.