
Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa yanazikanusha taarifa hizo za uzushi zenye lengo la kuwachanganya vijana wetu ambao wamehitimu mafunzo ya JKT na kurejea makwao.
Siku zote JKT imekuwa ikisisitiza kuwa vijana wanaojiunga na mafunzo ya JKT ni vyema wakatambua kuwa mafunzo hayo hayana uhusiano wa kupatiwa ajira kwenye vyombo vya ulinzi na usalama mara wamalizapo mkataba, bali mafunzo hayo yanawajengea uwezo wa kujuwa stadi za kazi na stadi za maisha.
Jeshi la Kujenga Taifa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wanafatilia kwa karibu kikundi kidogo chenye tabia ya kusambaza taarifa potofu na za uvumi zinazohusu J