Jengo la Mamlaka ya Bandari Bukoba lililokarabatiwa kuboreshwa na kuongezwa majengo mengine katika bandari hiyo.
………………………………………..
Katika sekeseke hilo tayari vijana walichanganyikiwa ndani ya gari wakadhani kimeshawaka wakakaa kimyaa, tukatembea kama mita 200 hivi ndiyo zikaanza kusikika sauti vicheko kidogo na mazungumzo, Hata hivyo kwa uwezo wa mwenyezi Mungu tuliingia mjini Bukoba tukiwa salama salimini.
Kaimu Meneja wa Bandari za Ziwa Victoria, Geofrey Lwesya akionesha moja ya viti vya kisasa vitakavyowekwa katika chumba cha abiria
………………………………………..
Siku iliyofuata Juni 6 tuliamka mapema tukapata supu ya Samaki wa kutosha kabisa ilipofika mida ya saa nne hivi tukaenda katika bandari ya Bukoba ambako tulikuwa na kazi ya kukagua jengo jipya lililokarabatiwa na kuongezwa majengo mengine hivyo kuwa la kisasa kabisa pamoja na mizani iliyojengwa bandarini hapo.
Jengo hili lilijengwa mwaka 1945 na lilikaa muda mrefu bila kukarabatiwa pamoja na huduma za bandari kuongezeka lakini bado watumishi walikuwa wakitumia jengo hilo kama ofisi na jengo hile kwa muda wote ambapo baadaye srikali ya awamu ya Tano iliamua kulikarabati na kuongeza majengo mengine.
Mradi huu Ukarabati wa Jengo la Ofisi na Abiria awamu ya pili Kwa sasa umefikia 95% ya utekelezaji wake. Mradi huu ulitegemewa kufanyiwa uaguzi wa mwisho tarehe 15.6.2019 na umegharibu kiasi cha shilingi milioni 143,856,160.00.
Kwa upande wa ujenzi wa Ujenzi wa Gati la Magarini Mradi huu Kwa sasa umefikia 62% ya utekelezaji. Sehemu ya kazi iliyokuwa imebaki ilikuwa kumalizia ujenzi wa Gati, jengo la abiria, jengo la mizigo, vyoo, mnara wa tenki la maji pamoja na ujenzi wa chumba cha mashine ya umeme pamoja na chumba cha walinzi. Mradi ulitarajiwa kukamilika 16.6.2019 unagharimu kiasi cha shilingi biioni 1,730,717,167.52.
Mkuu wa uhusiano wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera Sugar Bi. Shamsa Mohamed akizungumza katika bandari ya Bukoba.
………………………………………………..
Ningekuwa mwandishi mzuri wa vitabu kama waandishi wa vitabu Shafii Adam na kitabu chake cha “Vuta N”kuvute” au Bwana MSA na kitabu chake “Kosa la Bwana MSA” ningeweza kusimulia uzuri wa Bi. Shamsa Mohamed Mkuu wa uhusiano Kiwanda cha Sukari Kagera Sugar itoshe tuu kusema Dada Shamsa Kajaaliwa na Muumba wetu.
Akihojiwa na waandishi wa habari Mkuu huyo wa uhusiano Kiwanda cha Sukari Kagera Sugar Bi. Shamsa Mohamed akasema huduma wanazopewa na bandari wanapo safirisha au kupokea mizigo kupitia bandari ya Bukoba kwao limekuwa jambo zuri sana kwa sababu gharama za usafirishaji zinapungua.
Akasisitiza kwamba huduma hizo kwa sasa zimeboreshwa na kuwa zenye ufanisi zaidi kwa kuwa hutolewa masaa 24.
” Tangu tuanze kutumia usafiri wa majini tumegundua kwamba una unafuu mkubwa na tunasafirisha bidhaa zetu kwa wingi ukilinganisha na usafiri wa barabara ambao una gharama kubwa kwetu”
Mara nyingi wakati wa Mahojiano Kijana wangu Willy alikuwa anajitolea kushika vinasa sauti lakini Safari hii Kijana wangu mwingine Khaleed Gangana akaamua kujitosa kushika vinasa sauti akisema.
“Leo nashika mimi vipaza sauti mwenyewe ulikuwa upendo ulioje kwa kumsaidia kazi hiyo mdogo wetu Willy ambaye toka tulipoanza ziara ilikuwa kama ni kazi yake maalum, Hapa Gangana alionyesha upendo wa hali ya juu kwakweli ila sijui kama kulikuwa na la ziada baada ya kumuona Bi. Shamsa pengine ulikuwa ni upendo wake tu.
Basi tulipomaliza kazi ile moja kwa moja tulienda kula chakula huku Senene wakitafunwa vya kutosha, kisha baada ya kupata chakula cha mchana tukaondoka kuelekea mkoani Kigoma kuendelea na kazi ya kukagua miradi ya maendeleo katika bandari za ziwa Tanganyika.
Basi kama kawaida Dereva wetu Hassan Shaban aliwasha gari na kupiga gia safari ikawa imeanza huku utani wa hapa na pale ukiendelea, Lakini utani wa safari hii pia ulikuwa namna ya kuupita msitu wa Nduta ambao nao una habari yake tata kwa matukio yanayotokea wakati mwingine .
Maneno mengi yakaongelewa watu wakacheka na kuwaza lakini kila tulipofika umbali fulani tulikuta geti na askari wenye silaha dereva wetu Hassan alisimamishwa na kuulizwa mawili matatu na kumalizana nao kisha tuliendelea na safari.
Tulipofika Nyakahura jua lilikuwa limeshazama tukaamua kulala hapo ili tuondoke kesho asubuhi kuendelea na safari ya Kibondo- Kasulu mpaka Kigoma.
Kulipokucha niliamka mapema ili kujiandaa kisha nikaanza kuwapigia simu vijana wangu ili kuanza safari siku hiyo Kiongozi wa safari yetu Afisa Mawasilano wa (TPA) Bw. Leonard Magomba alikuwa amenikabidhi jukumu hilo, Sasa bwana nikampigia simu Kijana wangu mmoja Hirraly lakini duh! alikuwa mkali akanijibu hivi kwenye simu “Sisi tumechelewa kuamka tusubirini kama hamuwezi ondokeni” akisikika kama mtu mwenye usingizi mzito.
Basi kulingana na mazingira ya kazi nikaona vijana hawa wamechoka tukawasubiri kiasi baadaye walikuja tukaondoka, Sarafi ikaendelea, Maeneo mengi tuliyopita barabara nyingi wakandarasi walikuwa wakiendelea na ujenzi kuonyesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo unakwenda kwa kasi chini ya Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Jemedari wa mapambano Rais Dk. John Pombe Magufuli.
Tuliendelea na safari lakini bado vijana walikuwa na wasiwasi wa kupita msitu wa Nduta huko Kibondo jambo kubwa hapa nataka niishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kwa kazi kubwa inayofanya katika suala zima la usalama kiukweli tulikuwa na wasiwasi lakini kila tulipofika mahali tuliwakuta askari walitusimamisha na kutuuliza mawili matatu na walituambia tunatakiwa kuwa makini hapa tuliona kweli kuna kazi ya kuimarisha usalama inafanyika.
Kazi hii ya kuwalinda watanzania na mali zao si ndogo ni kubwa na ndiyo maana nachelea kupongeza serkali yetu na vyombo vyote vya ulinzi na usalama chini ya amiri jeshi Mkuu Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kuwasimamia vyema watendaji wake kwakweli askari wetu wanafanya kazi kubwa Hongereni sana makamanda.
Baadaye mchana tuliingia mjini Kasulu ambapo tuliamua kupata chakula cha mchana kwa sababu watu walikuwa na njaa sana tulipoingia kwenye mgahawa mmoja mjini hapo tulikuta baadhi ya vyakula bado havijaiva chakula kilichokuwa tayari ni Pilau nyama, Watu wakagonga pilau vya kutosha kisha tukaondoka hapo kuelekea Kigoma na kuwasili mida ya saa kumi hivi za jioni.
Baada ya hapo tukapokelewa na mwenyeji wetu dereva wa Port Manager wa Kigoma Kijana Essau alituongoza tukatafuta maeneo ya kufikia Mimi, Shayo na Mabere Makubi pamoja na dereva Hassan Shaban tukafikia Sumbawanga nitakueleza hii Sumbawanga ya wapi.
Vijana wangu Hirraly Willy, Gangana na rafiki yangu mkubwa Oscar wa Kasubi wakafikia lodge inaitwa (Excutive Food & Bed) siyo nimekosea kibao cha Lodge kimeandikwa hivyo jamani. FUATILIA SIMULIZI HII hapa ndipo anakuja Port Manager wa Kigoma Ajuaye Kheri Msese mtu makini katika kazi zake………………….
INAENDELEA
ENDELEA KUFUATILIA NITAKUSIMULIA MAAJABU YA RAIS MAGUFULI NILIYOYAONA.