Home Michezo ADDO KOMBA AZINDUA MASHINDANO YA MPIRA WA MIGUU,PETE YA BUCHIMWE CUP 2019...

ADDO KOMBA AZINDUA MASHINDANO YA MPIRA WA MIGUU,PETE YA BUCHIMWE CUP 2019 YALIYOANDALIWA NA DIWANI WA KATA YA BUIGIRI (CCM)

0

Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo Nchini, Addo Komba,akisalimiana na viongozi kabla ya uzinduzi rasmi wa mashindano ya Mpira wa Miguu na Mpira wa Pete ya Buchimwe Cup 2019 yaliyoandaliwa na Diwani wa Kata ya Buigiri (CCM) Mhe.Kenneth Yindi wilaya ya Chamwino.

Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo Nchini, Addo Komba,akitetea jambo na Diwani wa kata ya Buigiri Mhe.Kenneth Yindi wakati wa uzinduzi rasmi wa mashindano ya Mpira wa Miguu na Mpira wa Pete ya Buchimwe Cup 2019 yaliyoandaliwa na Diwani wa Kata ya Buigiri (CCM) wilaya ya Chamwino.

Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo Nchini, Addo Komba,akisalimiana na Afisa Elimu Kata ya Buigiri,Emmanuel Lotto baada ya kusoma risala fupi kabla ya  uzinduzi rasmi wa mashindano ya Mpira wa Miguu na Mpira wa Pete ya Buchimwe Cup 2019 yaliyoandaliwa na Diwani wa Kata ya Buigiri (CCM) (CCM) Mhe.Kenneth Yindi wilaya ya Chamwino.

Timu ya Buigiri Misheni wakiwa katika pozi la picha kabla ya kumenyana na Uguzi katika mashindano ya Buchimwe Cup 2019.

Kikosi cha timu ya Uguzi wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mpambano wao dhidi ya Buigiri Misheni Buchimwe Cup 2019.

Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo Nchini, Addo Komba akiwa katika picha ya pamoja na waamuzi kabla ya kuzindua  rasmi mashindano ya Mpira wa Miguu na Mpira wa Pete ya Buchimwe Cup 2019 yaliyoandaliwa na Diwani wa Kata ya Buigiri (CCM) wilaya ya Chamwino.

Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo Nchini, Addo Komba akiwa katika picha ya pamoja na Kikosi cha timu ya Uguzi FC  kabla ya kuzindua  rasmi mashindano ya Mpira wa Miguu na Mpira wa Pete ya Buchimwe Cup 2019 yaliyoandaliwa na Diwani wa Kata ya Buigiri (CCM) wilaya ya Chamwino.

Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo Nchini, Addo Komba akiwa katika picha ya pamoja na Kikosi cha timu ya Buigiri Misheni  FC  kabla ya kuzindua  rasmi mashindano ya Mpira wa Miguu na Mpira wa Pete ya Buchimwe Cup 2019 yaliyoandaliwa na Diwani wa Kata ya Buigiri (CCM) wilaya ya Chamwino.

Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo Nchini, Addo Komba akiwa katika picha ya pamoja na Kikundi cha ngoma kabla ya kuzindua  rasmi mashindano ya Mpira wa Miguu na Mpira wa Pete ya Buchimwe Cup 2019 yaliyoandaliwa na Diwani wa Kata ya Buigiri (CCM) wilaya ya Chamwino.

Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo Nchini, Addo Komba akizungumza na timu zote za Buigiri Misheni na Uguzi FC akiwa  kabla ya kuzindua  rasmi mashindano ya Mpira wa Miguu na Mpira wa Pete ya Buchimwe Cup 2019 yaliyoandaliwa na Diwani wa Kata ya Buigiri (CCM) wilaya ya Chamwino.

Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo Nchini, Addo Komba akipiga penalti kuashiria uzinduzi mashindano ya Mpira wa Miguu na Mpira wa Pete ya Buchimwe Cup 2019 yaliyoandaliwa na Diwani wa Kata ya Buigiri (CCM) wilaya ya Chamwino.

Wachezaji wakitivuana katika mpambano mkali kati ya Buigiri Misheni na Uguzi FC timu hizo zilitoka sare ya kufungana goli 1-1.

Diwani wa Kata ya Buigiri Mhe Yindi akitoa zawadi ya shilingi elfu tano kwa mchezaji bora wa mechi kutoka timu ya Buigiri Misheni katika mashindano ya Buchimwe Cup 2019.Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog

…………………..

Na.Alex Sonna,Buigiri,Dodoma

Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo Nchini, Addo Komba amezindua rasmi mashindano ya Mpira wa Miguu na Mpira wa Pete ya Buchimwe Cup 2019 yaliyoandaliwa na Diwani wa Kata ya Buigiri (CCM) wilaya ya Chamwino.

Mashindano hayo yanashirikisha Timu nane Kwa kila mchezo ambapo mshindi wa kwanza atajinyakulia Kombe, Seti Moja ya Jezi na kiasi cha Sh 100,000 taslimu.

Akizungumza wakati wa ufunguzi huo Komba amesema Serikali kupitia Wizara ya Michezo itaendelea kuunga mkono maendeleo ya Michezo kwani wanaamini licha ya Michezo kuwa ni Afya lakini siku hizi imekua ni Ajira ambayo imenufaisha kundi kubwa la vijana.

” Nimpongeze Diwani wenu, Mhe Yindi kwa kuandaa mashindano haya, kila mwaka amekua akianzisha Ligi mbalimbali kwa ajili yenu, hii ni faida kwenu na myatumie mashindano haya kukuza vipaji venu na kuhakikisha mnapiga hatua nyingine ya kupata Timu zinashoriki Ligi kubwa,” amesema Komba.

Nae Diwani wa Kata hiyo Mhe Yindi amesema pamoja na kuanzisha mashindano hayo pia kutakua na kozi za uamuzi kwa vijana waliomaliza kidato cha nne ambazo zitaendeshwa na wakufunzi kutoka Chama Cha Soka Mkoa wa Dodoma, (DOREFA).

” Lengo la mashindano haya ni kuhakikisha vijana wetu wanapiga hatua, lakini pia kuunga mkono juhudi za Mhe Rais Dk John Magufuli kukuza sekta ya Michezo nchini, na sisi kama watu tunaomsaidia inatubidi kumuunga mkono kwa vitendo.

” Tunafahamu kuwa mna changamoto ya viwanja vya kuchezea, nimeshaanza kushughulikia na nina hakika kupitia Wizara ya Michezo tutamaliza changamoto hiyo,” amesema Mhe Yindi.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Chinonwa, Mhe Joel Mwaka amempongeza Diwani Yindi kwa kuandaa mashindano hayo na kuahidi kutoa mchango wake wa hali na mali katika kila hatua ya mashindano hayo.

Nao wananchi wa Kata hiyo wamemshukuru Diwani huyo kwa kudhamini upatikanaji wa Jezi na Mipira kwa kila timu zinazoshiriki Ligi hiyo kwani kumeongeza ari ya kufanya vema.