Mjasiliamali na muhitimu wa Chuo Kikuu cha Da es Salaam, Bw. Moi Masombe akionyesha chati ambayo ikionyesha ni namna gani nyuzi za katani pori zilivyokuwa bora katika matumizi.
Moja ya katani pori ambayo inatengeneza malighafi ambazo zinaweza kusaidia kupata vitu mbalimbali kama kamba pamoja na samani mbalimbali na pia hutumika kama pambo
Nyuzi za katani pori zilizopo tayari kwaajili ya matumizi baada ya kuchakatwa na kuwa nyuzi kutoka katika katani
Moja ya kifaa ambacho kimetengezwa kwa kutumia malighafi ya katani pori
**************
Katani pori maalufu wild sisal inauwezo wa kutengeneza bidhaa ambazo ni ngumu na imara kwa matumizi kwani nyuzi zake ni ndefu na ngumu mbazo zinahimili kufanya kazi ambazo zitahitaji kamba au nyuzi za katani katika matumizi.
Ameyasema hayo leo Mjasiliamali na muhitimu wa wa Chuo Kikuu cha Da es Salaam, Bw. Moi Masombe katika maonyesho ya biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika maonyesho hayo Bw. Masombe amesema kuwa wanaweza kuzalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo makapeti pamoja na kamba kama katani ya kawaida lakini utofauti wake ni ubora.
“Kuna baadhi ya watu hutumia kama mapambo lakini mara nyingi huota katika maeneo ya porini kwa wingi. Hivyo watu wangeweza kutumia fursa hii kutengeneza bidhaa zilizobora kwa kutumia katani pori”. Amesema Bw.Masombe.
Amesema kuwa urefu wa nyuzi za katani poli ni sm 138 wakati katani za kawaida mara nyingi urefu wake ni sm 60 mpaka sm 90 hivyo ni bora kwa matumizi Zaidi ya zile za kawaida ambazo wengi wamezizoea kuzitumia.