**********
Na Stahmil Mohamed
Ofisi ya Waziri Mkuu Inayoshughulika na Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu imeanza operesheni maalumu ya ukaguzi wa miradi katika halmashauri na mikoa mbalimbali nchini lengo ni kutathimini utekelezaji wa programu za maendeleo za vijana na kuona changamoto zinazowakabili na kubaini fursa mbalimbali zilizopo Nchini.
Akizungumza na waandishi Wa Habari Kaimu Mkurugenzi Ukuzaji Bibi. Venerose Mtenga amesema operesheni hii imeanza rasmi juni 11 lengo ni kuona na kukagua miradi mbalimbali , kuona changamoto za vijana na kubaini fursa zilizopo katika mikoa na Wilaya pia kuandaa mkakati mzuri na wapamoja namna ya kutatua changamoto na kuandaa mkakati wa namna ya kuratibu shughuli za kuwezesha vijana kiuchumi.
Aidha Bi. Venerose amesema katika zoezi hilo pamoja na mambo mengine wataalamu mbalimbali watatembelea na kukagua miradi ya uzalishaji mali ya vikundi vya vijana pamoja na kutathimini hali halisi ya utekelezaji programu za kuwezesha makundi mbalimbali yakiwemo wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Hata hivyo Bi. Venerose amebainisha katika tathimini inalenga kufuatilia marejesho ya fedha zilizokopeswa kwa vijana kupitia mfuko wa maendeleo wa vijana pia itatoa fursa kwa wadau mbalimbali wa masuala ya maendeleo walioshiriki katika programu za kuwawezesha vijana kupendekeza namna nzuri ya kuboresha mahusiano na ushirikiano kwa jamii.
Pia Bi. Venerose ameongeza kwa kusema kuwa miradi inayotembelewa ni miradi ya kilimo cha umwagiliaji kwa teknolojia ya kitalu nyumba unaotekelezwa na halmashauri zote nchini, mabwawa ya samaki ,ushonaji, ufugaji nyuki, pamoja na uchomeleaji vyuma.
Akizungumzia upande wa changamoto bi. venerose amesema kwa baadhi ya sehemu walizofanya zara marejesho ya mikopo kwa upande wa vijana ni changamoto kubwa kutokana na baadhi ya vijana wanapokabidhiwa mikopo hiyo wanahama maeneo hivyo hupelekea suala la marejesho kuwa gumu na baadhi ya vikundi kusambaratika jambo ambalo limeonesha vijana sio waamifu ukilinganisha na makundi ya wanawake .akiongeza changamoto nyingine ni mabadiliko ya hali ya hewa ya mwaka huu yameongeza changamoto kubwa kwa baadhi ya vikundi vilivyojikita katika kilimo kwani vijana wamesema wameshindwa kutekeleza miradi kwa ufanisi.
Ucheleweshwaji wa mikopo, na fedha ya mikopo inayotoka imeelezwa kuwa pia nichangamoto kubwa kwani haikidhi mahitaji na kusababisha kutokufanikiwa kwa malengo ya miradi. Pia elimu ya ujasiliamali pamoja na uwepo wa masoko ya bidhaa vinachochea kudorola kwa vikundi.
Bi. Ameainisha kuwa mafanikio kwa baadhi ya vikundi vilivyokopeshwa ma alivyotembelea katika baadhi ya mikoa kama Singida na Dodoma wameweza kukuza mitaji na kujenga uwezo kama ilivyokusudiwa jambo lililopelekea kuaminika na kupewa Zabuni mbalimbali hasa vikundi vya upande wa wanawake kiasi cha kuwasaidia wanawake wengi hadi sasa wamefanikiwa kulipa ada za watoto mashuleni na kuboresha lishe na ustawi wa familia kwa ujumla hali iliyowafanya kuwajengea kujiamini zaidi kutokana na kuondokana na utegemezi kwa familia zao.