Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa
Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi 
 (AQRB) 
Arch. Dkt Ludigija Bulamile akifungua  mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishishi wa habari  Jijini Dar es Salaam yaliyoandaliwa na bodi hiyo kuhusu kuacha kuichanganya
taaluma yao na ile ya wahandisi    badala yake iuelimishe umma
tofauti iliyopo baina ya taaluma hizo mbili na umuhimu wa kuwatumia wataalamu
hao wanapofanya ujenzi.

(PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON)

  Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) Arch.Albert Munuo, akisoma taarifa kuhusu majukumu ya bodi hiyo (kulia) Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Ludigija Bulamile.

 Afisa Mkuu wa Sheria Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) Ibrahim Mohamed akielezea makosa mbali mbali ya
kisheria yanayofanywa yakiwemo yale ya uuzwaji wa ramani hadharani pasipo
kufuata taratibu. 

  Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi  (AQRB) Arch . Dkt Ludigija Bulamile akipitia taarifa mbali mbali za bodi hiyo.

 Watumishi wa bodi hiyo wakiwa katika  mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishishi wa habari  yaliyoandaliwa na bodi hiyo kuhusu kuacha kuichanganya taaluma yao na ile ya wahandisi    badala yake iuelimishe umma tofauti iliyopo baina ya taaluma hizo mbili na umuhimu wa kuwatumia wataalamu hao wanapofanya ujenzi.

 Afisa Mdhibiti Mwandamizi wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi  (AQRB) Mlezi Makuka (kushoto aliyesimama) akichangia mada yake wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishishi wa habari  yaliyoandaliwa na bodi hiyo kuhusu kuacha kuichanganya taaluma yao na ile ya wahandisi    badala yake iuelimishe umma tofauti iliyopo baina ya taaluma hizo mbili na umuhimu wa kuwatumia wataalamu hao wanapofanya ujenzi.

 Arch. Mbaraka Igangula akichangia mada.

 QS.Mashaka Bundara akisisitiza jambo.

  Arch.Joseph Ringo akichangia mada wakati wa mafunzo hayo.

 Waandishi wa Habari wakichangia mada mbali mbali wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo  yaliyoandaliwa na Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi  (AQRB) kuacha kuichanganya taaluma yao na ile ya wahandisi    badala yake iuelimishe umma tofauti iliyopo baina ya taaluma hizo mbili na umuhimu wa kuwatumia wataalamu hao wanapofanya ujenzi.

  Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi  (AQRB) Dkt. Ludigija Bulamile akijibu maswali.

Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi  (AQRB) Dkt. Ludigija Bulamile,  Kaimu Msajili  Albert Munuo pamoja na waandishi wa habari na wajumbe wa bodi hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi  (AQRB) 

………………………………………….

BODI ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi
(AQRB) imewataka wanahabari nchini  kuacha kuichanganya taaluma yao na ile
ya wahandisi    badala yake iuelimishe umma tofauti iliyopo baina ya
taaluma hizo mbili na umuhimu wa kuwatumia wataalamu hao wanapofanya ujenzi.
Akizungumza alipokuwa akifungua   mafunzo ya
kuwajengea uwezo waandishishi wa habari  yaliyoandaliwa na menejimenti ya
bodi hiyo mwishoni  mwa wiki Jijini Dar es salaam   Mwenyekiti
wa AQRB  Dkt. Ludigija Bulamile alisema lengo ni kuwaelimisha waandishi
shughuli na majukumu yake katika sekta ya ujenzi ili waweze kuuelimisha umma wa
watanzania faida na hasara za kutowatumia wabunifu majengo na wakadiriaji
majenzi wanapofanya ujenzi wowote. 
 Alisema kumekuwa na mkanganyiko  wa utoaji taarifa
unaofanywa na waandishi wakati wanaripoti masuala yanayohusu  taaluma hizo
hivyo  ili kuondoa mkanganyiko huo wanahabari wana kila sababu ya
kuyatumia mafunzo haya kwa kuwaelimisha wengine  kuzitumia kalamu zao
kuuelimisha umma tofauti za taaluma hizo.
‘EIelimisheni jamii  umuhimu wa kuwatumia wabunifu majengo
na wakadiriaji majenzi katika ujenzi ili waweze kupata makazi  bora,
ambayo pia yatawapa nafuu kwenye gharama za ujenzi kulingana na
matakwa,’.alisema Bulamile.  
Aliongeza kufafanua zaidi sababu za wahandisi kufahamika zaidi
na umma kuliko wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi pamoja na kufanya kazi
zinazoshabihiana kuwa ni pamoja na  taaluma hiyo kuchelewa kuingia
nchini.   
” Mpaka sasa nchi nzima ina   wataalamu wa
taaluma hii  wasiozidi 1,500 hili bado ni tatizo kulingana na idadi ya
watu na mahitaji yake,” alisema Dkt. Bulamile  na kuongeza bodi
imeendelea kuongea na baadhi ya vyuo vikuu vilivyopo nchini vione umuhimu wa
kufundisha taaluma hii ili kuongeza idadi ya wataalamu watakaowezesha kuibadili
sura ya nchi hapo baadae katika sekta ya ujenzi  kwa kubuni majengo ya
kisasa yanayoendana na wakati.
 Kwa upande wake Kaimu Msajili wa bodi Mkadiriaji Majenzi
Albert Munuo alisema kuwa,pamoja na kusajili wataalamu wa fani hiyo na
makampuni pia wanamajukumu ya kukagua miradi ya ujenzi inayoendelea ili kuona
kama wataalamu wamehusika.
” Tumekuwa tukikagua ujenzi wa miradi mbalimbali
mikubwa inayoendelea na kwamba kwa sasa tunajipanga kuutembelea mradi wa ujenzi
wa reli ya kisasa SGR ili kujionea ni kwa namna gani Wabunifu Majengo na
Wakadiriaji Majenzi wameshiriki ,’alisema  Munuo
Aliongeza kuwa AQRB ni taasisi ya serikali iliyopo chini ya
Wizara ya Ujenzi na kwamba mpaka sasa ina ofisi katika kanda tano ikiwepo Kanda
ya Mashariki, kanda ya ziwa, kanda ya kaskazini ,nyanda za juu kusini na kanda
ya kati. 
Mafunzo hayo pamoja na kuhudhuriwa na baadhi ya waandishi kutoka
vyombo mbalimbali zikiwepo televisheni, redio na magazeti pia wataalamu wengine
wa ujenzi kutoka AQRB akiwepo mwanasheria wao alishiriki na kusema yapo makosa
mbali mbali ya kisheria yamekuwa yakifanywa ikiwepo lile la uuzwaji wa ramani
hadharani pasipo kufuata taratibu. 

Hata hivyo wataalamu hao waliongeza kutolea mfano kwa kusema asilimia
90 ya nyumba zilizojengwa Dar es salaam zimejengwa bila vibali na kusababisha
hasara kwa jamii pale ambapo eneo hilo linapokuja kubainika kuwa si
mahali  sahihi kwa ujenzi wa makazi na kulazimika kubomolewa.