WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwele akipata maelezokutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA Injinia Deusdedit Kakoko wakati alipotembelea kukagua mizani ya Shimo la Udongo ambako kulilipotiwa mgomo wa madereva wa malori kuanzia jana mchana mpaka usiku.
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwele maelekezo kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA Injinia Deusdedit Kakoko wakati alipotembelea kukagua mizani ya Shimo la Udongo ambako kulilipotiwa mgomo wa madereva wa malori kuanzia jana mchana mpaka usiku.
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwele akiongozana na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA Injinia Deusdedit Kakoko wakati alipotembelea kukagua mizani ya Shimo la Udongo ambako kulilipotiwa mgomo wa madereva wa malori kuanzia jana mchana mpaka usiku.
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwele akikagua mizani ya Shimo la Udongo wakati alipotembelea kukagua mizani ya Shimo la Udongo ambako kulilipotiwa mgomo wa madereva wa malori kuanzia jana mchana mpaka usiku.
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwele akipata maelezokutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA Injinia Deusdedit Kakoko na wasimamizi wa mizani hiyo wakati alipotembelea kukagua mizani ya Shimo la Udongo ambako kulilipotiwa mgomo wa madereva wa malori kuanzia jana mchana mpaka usiku.
……………………………………………..
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwele amewapiga mkwara mzito Wamiliki wa kampuni zinazoendesha bandari kavu(ICDS) kwa tuhuma za kuhamasisha mgomo wa malori bandarini.
Waziri Kamwelwe amepiga mkwara huo baada ya kampuni hizo kutuhumiwa kuhamasisha madereva wa malori yanayotoa mizigo bandarini kufanya mgomo kuanzia jana mchana hadi usiku kwa lengo la kuondolewa kwa mizani ya kupima uzito wa magari hayo kabla ya kuanza safari zake kwa njia ya barabara.
Waziri Isack Kamwele, ameongeza kuwa atazichukulia hatua kampuni hizo kwa kuzinyima leseni zilizoomba leseni kwa ajili ya kuendesha bandari kavu(ICDS) kwa tuhuma za kuhamasisha mgomo wa malori bandarini.
Kamwele ameyaeleza hayo leo, alipofanya ziara ya kukagua mizani hizo kuona kama inasababisha foleni kama ilivyodaiwa na baadhi ya wafanyabiashara hao na kubaini kuwa lori moja linachukua sekunde 55 hadi dakika moja kupimwa uzito.
“Niliona ni lazimakuja kuona ukweli kama hizi mizani zinasababisha foleni, lakini si kweli kwa sababu kuna mizani mbili na zote ni nzima na wanatumia si chini ya dakika moja kupima na kuondoka eneo hili”.
Tumeshabaini waliohusika kufanya mgomo huu ni kampuni tatu ikiwamo PrimeFuel ambao tunawaita ni ‘Wahaini’ kwa sababu lengo lao ni kukwamisha miradi ya Serikali na waliomba leseni za ICDS sasa tutawaonyesha kama sisi ni Serikali na walichofanya si sahihi” amesema Kamwele.
Ameeza zaidi kuwa, leseni ya wafanyabiashara wa ICDS zinatoka Julai 17 na wafanyabishara waliohusika kufanya hujuma hizo hawatapatiwa leseni zao kwa sababu wanakwamisha juhudi za Rais John Magufuli. katika kuiletea nchi maendeleo