Baadhi ya watoto walionaswa na kamera ya BMG wakicheza katika korongo hatari la Bolelo lililopo Kata ya Kumsenga, Halmashauri ya Mji wa Kasulu mkoani Kigoma ambapo korongo hilo linaelezwa kuwa uwanja wa vitendo viovu ikiwemo ushirikina.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Pia korongo la Bolelo licha ya kwamba ni hatari kwa jinsi lilivyo, bado linapendwa na watoto wakiwemo wanafunzi wa shule za msingi zilizopo jirani ambapo wamekuwa wakilitumia kwa kucheza/ kujificha wanapotoroka shuleni.
Nyakati za usiku inaelezwa korongo hili ni hatari kwa wakazi wanaokatisha hapa kwani baadhi ya wahalifu hulitumia kufanya uhalifu kama vile ukabaji.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwenge wilayani Kasulu, Mwl. John Edson akieleza mbele ya wanahabari namna uwepo wa korongo la Bolelo jirani na shule hiyo unavyoathiri masomo kwa wanafunzi ambao wamekuwa wakitoroka na kwenda kujifisha humo.
Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Watoto na Wanawake KIVULINI, Yassin Ally (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Shule ya Msingi Mwenge, Mwl. John Edson kuhusiana na mathara ya korongo ya Bolelo kwa wanafunzi.