Waziri wa Ujenzi,Uchukukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe akiongea na baadhi ya viongozi ambao wanasimamia ujenzi wa nyumba zilizopo Magomeni Kota kwa wale ambao walivunjiwa nyumba zao kupisha ujenzi wa nyumba hizo kama agizo lilivyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli
Baadhi ya Majengo ambayo yanaendelea kujengwa katika maeneo ya Magomeni Kota kwa wale ambao walivunjiwa nyumba zao kupisha ujenzi wa nyumba hizo kama agizo lilivyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli.
Baadhi ya Nyumba zilizopo Bunju B kwaajili ya kuuzwa au kukopeshwa na zilijengwa kwaajili ya watumishi wa Serikali kabla Serikali haijaamia Dodoma.
***************
NA EMMANUEL MBATILO
Waziri wa Ujenzi,Uchukukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amemuagiza Katibu Mkuu wa Wakala wa Majengo (TBA) ambaye anasimamia ujenzi kuhakikisha anampelekea majina ya wasimamizi wa miradi yote ya Ujenzi nchi nzima ili kuanagalia utaalamu walionao.
Ameyasema hayo leo baada ya kutembelea ujenzi wa nyumba zinazojengwa maeneo ya Magomeni Kota kwaajili ya kaya 644 ambapo kufikia mwezi Desemba utakuwa umekamilika.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Waziri huyo amesema kuwa hajafurahishwa na maendeleo ya ujenzi huo kwani hawaendi na wakati hasa ujenzi huo kwenda taratibu.
“Kwanini msiingie mkataba na watu wa kokoto, mchanga ili ujenzi uendelee alafu mnanieleza kuwa ukosefu wa fedha ndo chanzo cha ujenzi huo kwenda taratibu”. Amesema Mhandisi Kamwelwe.
Aidha Waziri Kamwele amewapa pongezi Wakala wa Majengo (TBA) kwa hatua waliofikia katika kukamilisha ujenzi wa majengo yaliyopo Bunju B nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ambapo majengo hayo yalijengwa kwaajili ya Watumishi wa Serikali hivyo kwasasa nyumba hizo zinauzwa na kukopeshwa.
Naye Msanifu Majengo Hamisi Kileo amesema kuwa ukosefu wa rasilimali fedha zimefanya ujenzi huo kutokukamilika kwa wakati kwani amedai fedha hizo wakizipata mradi utakamilika kwa wakati.