***********
NA EMMANUEL MBATILO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametoa ruhusa kwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kusafiri kwenda Misri kuwapa motisha wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
Ameeleza hayo leo wakati akizindua Ghala na Mitambo ya Gesi ya LPG ya Taifa Gas Tanzania Limited katika eneo la Vijibweni Kigamboni Jijini Dar es salaam.
“Makonda umesema ukienda Misri Taifa Stars tutashinda kutokana na motisha ya ushangiliaji, panda ndege nenda si umesema tutashinda nenda” amesema Rais Magufuli.
Awali RC Makonda alisema, “Vijana walikata tamaa kabisa na nimeongea nao jana usiku na leo asubuhi nimeongea na Sammata, nimewaambia tumuoneshe Mh.Rais ya kwamba tupo pamoja naye,hata kama tumedondoka na Senegal lakini tunanyanyuka na Wakenya lazima watakiona na wamenihakikishia Wakenya hawatoki,”.