***************

Beki Gerson Vieira aliyezungumzwa sana wiki iliyopita hatimaye leo ametambulishwa rasmi kuwa mchezaji halali wa Simba baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili

Vieira ambaye amewahi kuwa nahodha wa timu ya Taifa ya wachezaji chini ya miaka 17 ya Brazil, anamudu vyema nafasi ya beki na kiungo mkabaji

Kiraka huyo amewahi kucheza na wachezaji maarufu kama Neymar, Philippe Coutinho, Casemiro na golikipa Alisson, pia alicheza timu ya Taifa ya wachezaji chini ya miaka 20 na alicheza klabu kadhaa za Brazil ikiwepo Gremio

Ametua Simba akitokea klabu ya ATK FC inayoshiriki ligi kuu ya India