Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya AGPAHI, Bi. Asha Mtwangi akifungua kambi ya watoto na vijana kutoka mikoa ya Mara, Mwanza, Shinyanga na Simiyu inayofanyika jijini Dar es salaam.
***
Watoto na vijana wanaoishi na Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) wametakiwa kuzingatia matumizi sahihi ya dawa za kupunguza makali ya VVU ‘ARV’ ili waweze kuboresha afya zao hivyo kutimiza ndoto zao za maisha.
Wito huo umetolewa leo Jumapili Juni 23,2019 na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya asasi inayolenga kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia, Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI), Bi. Asha Mtwangi alipokuwa akifungua kambi ya watoto na vijana kutoka mikoa ya Mara, Mwanza, Shinyanga na Simiyu.
Katika kambi hiyo maarufu kama Ariel Camp inayofanyika katika hoteli ya Landmark, Mbezi Beach, Jijini Dar es salaam, Bi. Mtwangi alisema kama ilivyo kwa watoto wasio na VVU, watoto wanaoishi na VVU wana haki zote za kuishi, kupendwa, kusoma na kucheza.“Kuwa na maambukizi ya VVU hakuhalalishi kumnyima mtoto haki zake hizo,” alisisitiza.
Aidha Bi. Mtwangi aliipongeza AGPAHI kwa juhudi ambazo imekuwa ikizifanya kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za VVU na UKIMWI kwa watu wanaoishi na VVU.
“Matarajio yetu na ndoto zetu ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2022 kusiwe na mtoto mwenye UKIMWI,” alisema.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa, alisema kambi hiyo ni ya 13 tangu asasi hiyo ianzishe utaratibu wa kukutanisha watoto wanaotoka kwenye klabu za vijana zilizopo katika vituo vya huduma na matunzo vilivyopo kwenye mikoa ambayo AGPAHI inafanya kazi.
“Katika kambi hizi watoto wamekuwa wakibadilishana mawazo, kutiana moyo, kujifunza masuala ya VVU/UKIMWI, kukua, ujinsia na ujasiriamali. Pia wamekuwa wakijengewa ujasiri na kujiamini ili waweze kutimiza ndoto zao,” alisema.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya AGPAHI, Bi. Asha Mtwangi akizungumza wakati kifungua kambi ya watoto na vijana kutoka mikoa ya Mara, Mwanza, Shinyanga na Simiyu. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa.Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za mama na mtoto AGPAHI, Dk. Akwila Temu akifuatiwa na Mkurugenzi wa Taarifa za Takwimu,Utafiti na Ufuatiliaji wa AGPAHI, Dk. Boniphace Idindili. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde1 blog
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya AGPAHI, Bi. Asha Mtwangi akifungua kambi ya watoto na vijana kutoka mikoa ya Mara, Mwanza, Shinyanga na Simiyu na kuwataka vijana kutokata tamaa katika maisha.
Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa akizungumza wakati wa ufunguzi wa Ariel Camp 2019.
Vijana wakitoa burudani wimbo wakati wa ufunguzi wa Ariel Camp.
Burudani ya nyimbo ikiendelea ukumbini.
Viongozi wa AGPAHI wakifuatilia matukio wakati wa ufunguzi wa Ariel Camp.
Mtaalamu wa mambo ya sanaa kutoka kundi la Baba Watoto, Bw. Mkude Kilosa akicheza na vijana wanaoshiriki Ariel Camp.
Picha ya pamoja Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya AGPAHI, Bi. Asha Mtwangi na Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa,wafanyakazi wa AGPAHI na Baba watoto na washiriki wa Ariel Camp 2019 kutoka mikoa ya Mara, Mwanza, Shinyanga na Simiyu.
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde1 blog