*******************
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Liberatus Sabas, mapema leo
amefunga mafunzo katika Eneo la mafunzo liliopo Kilelepori wilayani
Hai mkoani Kilimanjaro kwa askari wanaotunza Silaha na Vielelezo
vilivyopo ndani ya vituo vya polisi katika sehemu mbalimbali, katika
hatua hiyo amewataka Askari kutenda kazi kwa kuzingatia Maadili na
Weledi ili kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi hii itasaidia
kuepuka kupotea kwa vielelezo hivyo.
Aidha katika hatua hiyo amewaonya Askari Polisi wanaoomba na
kupokea rushwa kutoka sehemu mbalimbali hasa kwa
wafanyabiashara na watu wengine wenye nia njema ya kuhakikisha
Uchumi wa Nchi unapanda na kufikia uchumi wa kati, Jeshi la Polisi
halitamuonea muhali askari yoyote bali atachukuliwa hatua kali za
kisheria ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi kisha kufikishwa
mahakamani kwa kufanya hivyo Jeshi la Polisi litakuwa limemuunga
mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Joseph
Magufuli katika kuhakikisha nchi yetu inafikia uchumi wa kati.
Amemalizia kwa kuwataka wale wote wanaotaka kuvunja amani au
kuchezea amani ya nchi yetu watachukuliwa hatua kali ili kuhakikisha
nchi inaendelea kuwa na amani kama ilivyo na inavyofahamika kuwa
Tanzania ni kisiwa cha amani.