Baadhi ya watoto waliofika kupata chanjo katika zahanati ya kijiji cha Kikonko katika halmashauri ya Mpimbwe
Baadhi ya kinamama na watoto wao wakisubiri chanjo katika zahanati ya Kikonko
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dk. Omary Sukari akitoa matone ya Vitamini A kwa mtoto
Watumishi wa halmashauri wakitumia usafiri wa pikipiki katika kufuatilia zoezi la chanjo linavyoendelea katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma
*********************
21.06.2019
Na Mwandishi wetu, Katavi
Jumla ya watoto 7,935 wa Halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoani Katavi watarajiwa kupata matone ya Vitamini A na dawa za minyoo katika zoezi la utoaji chanjo kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano linatalotarajiwa kukamilika juni 30 mwaka huu
Akizungumzia zoezi hilo Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mpimbwe dk. Sebastian Siwale amesema zoezi hilo litahusisha vituo 15 vya kutolea huduma za afya katika halmashauri hiyo
Aidha ameongeza kuwa wanakabiliwa na changamoto ya uchache wa vyombo vya usafiri hali inayopelekea wakati mwingine kushindwa kufuatilia kwa karibu jinsi zoezi hilo linavyoendelea katika vituo mbalimbali
“Tuna gari moja kwahiyo inapotokea kuna mgonjwa inabidi atumie gari hilo kupelekwa hospitali na ufuatiliaji unaahirishwa mpaka gari litakaporejea” alisema dk. Siwale
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi dk. Omary Sukari ambaye alikuwa ameambatana na kamati ya usimamizi wa huduma za afya mkoa wameshiriki katika zoezi hilo ambapo amesisitiza umuhimu wa watoto kupata chanjo
Dk Sukari amesema matone ya Vitamin A yanasaidia kinga ya mwili wa mtoto dhidi ya maradhi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kumwezesha mtoto kuona vizuri
Pia ametoa wito kwa wazazi waliowafikisha watoto wao kupata chanjo kuwa mabalozi wazuri kwa majirani zao ili watoto waote wapate chanjo hiyo
Nao baadhi ya kinamama waliokutwa katika vituo vya kutolea huduma ya afya wameeleza umuhimu wa chanjo hiyo ikiwa ni pamoja na kumpa mtoto kutibu minyoo inayoshambulia katika tumbo la mtoto